“What is bad luck? Opinion. What are conflict, dispute, blame, accusation, irreverence, and frivolity? They are all opinions, and more than that, they are opinions that lie outside of our own reasoned choice, presented as if they were good or evil. Let a person shift their opinions only to what belongs in the field of their own choice, and I guarantee that person will have peace of mind, whatever is happening around them.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.3.18b–19
Ni siku nyingine mpya kwetu wanamafanikio,
Tumeipata nafasi hii nzuri na ya kipekee sana kweru kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari PUNGUZA MAONI…
Siku hizi, kila mtu ana maoni kwenye kila jambo.
Mtu mmoja ana maoni yake kuhusu siasa, michezo, uchumi, afya, mahusiano, wasanii na mengine mengi.
Linapotokew jambo lolote, watu hawawezi kutulia bila ya kutoa maoni yao.
Tena wengine wanaona wamekosewa pale ambapo hawaulizwi maoni yao, au maoni yao hayafanyiwi kazi.
Rafiki, kama tunavyojua, maoni siyo ukweli, bali ni upendeleo tulionao sisi, kulingana na mtazamo wetu. Wakati mwingine tunakuwa tumebeba tu maoni hayo kutoka kwa wengine.
Hivyo kadiri unavyokuwa na maoni mengi, kadiri unavyokuwa na maoni kwenye kila jambo, ndivyo unavyozidi kujipa mzigo, ndivyo unavyozidi kujisumbua.
Suluhisho ni kupunguza maoni unayokuwa nayo, kuacha kuwa na maoni kwenye kila jambo.
Chagua kuwa na maoni kwenye yale mambo unayoyajua kweli na umebobea.
Chagua kuwa na maoni kwenye yale mambo ya muhimu kwako na yanayokufikisha kule unakokwenda.
Na mambo mengine yote ambayo hayaingii kwenye wigo wako, adhana nayo.
Usione vibaya kusema sina maoni.
Kutokuwa na maoni siyo ujinga, bali ni kujitambua na kujiheshimu.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kupunguza maoni unayokuwa nayo kwenye kila eneo la maisha.
#MaoniSiyoUkweli, #PunguzaMaoni, #KutokuwaNaMaoniSiyoUjinga
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha