“Those who receive the bare theories immediately want to spew them, as an upset stomach does its food. First digest your theories and you won’t throw them up. Otherwise they will be raw, spoiled, and not nourishing. After you’ve digested them, show us the changes in your reasoned choices, just like the shoulders of gymnasts display their diet and training, and as the craft of artisans show in what they’ve learned.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.21.1–3

Mimi na wewe ni nani mpaka tumeipata bahati hii nyingine nzuri ya kuiona siku hii mpya?
Je ni kwa sababu mimi na wewe tu wajanja sana?
Au kwa sababu tunastahili zaidi ya wengine?
Majibu ni hapana, hatuna ujanja sana wala hatustahili zaidi ya wengine,
Bali wajibu wetu hapa duniani bado haujakamilika, hivyo tunapaswa kutumia muda tunaopata kama leo, kikamilisha yale muhimu kwetu.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari ONESHA VITENDO NA SIYO MANENO…
Mtu anayenyanyua vyuma vizito hahitaji kukuambia kwamba ananyanyua vyuma vizito, utaona misuli yake ikionesha wazi kwamba mtu huyo ananyanyua vyuma vizito.
Mtu anayeishi kwa misingi bora ya afya hahitaji kukuhubiria namna anavyoishi maisha yake, bali utaona afya yakr ikiwa imara na utajua kuna kitu cha tofauti anafanya kinachoboresha afya yake.
Mtu anayeishi kwa misingi ya falsafa hahitaji kukushawishi kwa maneno uelewe falsafa yake, kwa maamuzi anayofanya na misimamo anayokuwa nayo itaonesha wazi ni mtu wa falsafa.

Rafiki, kwenye dunia hii ambayo kila mtu anapiga kelele, usijihangaishe kusikiliza mwenye kelele kubwa, badala yake angalia matokeo kwenye maisha yake.
Kama mtu anapiga kelele kubwa, lakini matokeo kwenye maisha yake ni tofauti na kelele anazopiga, amini matokeo nw puuza kelele.
Kadhalika kwenye maisha yako, unapopata msukumo wa kuwaambia watu kuhusu mambo yako, jiulize je hakuna matendo wanayoweza kuona wao wenyewe?
Na kama yapo basi funga mdomo na acha matokeo yaongee.

Hii pia ni njia bora ya kuwafundisha na hata kuwabadilisha watu, usiwaambie nini cha kufanya, bali waoneshe nini cha kufanya.
Matendo yana uzito kuliko maneno, tumia zaidi matendo.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuonesha matendo na kuachana na kelele.
#OneshaMatokeo, #AchaManenoWekaKazi, #MtendoYanaNguvuKulikoManeno

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha