“God laid down this law, saying: if you want some good, get it from yourself.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 1.29.4

Ni siku nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari JINSI YA KUWA NA SIKU BORA…
Kama unataka kuwa na siku bora, basi fanya yale yaliyo bora kwako.
Hakuna mtu yeyote anayeweza kuifanya siku yako kuwa bora isipokuwa wewe mwenyewe.
Chochote kizuri unachotaka, anza kukiangalia ndani yako, maana hakuna kitu cha nje ambacho unaweza kukitegemea kwa asilimia 100.

Unao uwezo wa kufanya makubwa sana kwenye maisha yako kama utautambua na kuutumia.
Unacho kila unachohitaji ili maisha yako yawe bora kama utajitambua na kutumia kila ambacho tayari unacho.

Kwa kadiri unavyotegemea machache ya nje, ndivyo unavyokuwa huru zaidi na maisha yako.
Kama unataka kuwa na siku bora, fanya yake yaliyo bora.
Kama unataka maisha mazuri, ishi vizuri.
Kama unataka uhuru mkubwa kwenye maisha yako, tegemea vitu vichache sana kutoka nje yako.

Ukawe na siku bora saba ya leo, kwa kuchagua kufanya yale ambayo ni bora zaidi kwako na kutegemea zaidi yaliyo ndani yako na siyo nje.
#UboraWaMaishaNiKuwaBora, #UhuruNiKujitegemea, #UnachoKilaUnachohitajiIliKuwaBora

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha