“If you don’t wish to be a hot-head, don’t feed your habit. Try as a first step to remain calm and count the days you haven’t been angry. I used to be angry every day, now every other day, then every third or fourth . . . if you make it as far as 30 days, thank God! For habit is first weakened and then obliterated. When you can say ‘I didn’t lose my temper today, or the next day, or for three or four months, but kept my cool under provocation,’ you will know you are in better health.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.18.11b–14

Ni siku nyingine mpya,
Siku nzuri na ya kipekee wana kwetu.
Ni nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USIVUNJE MNYORORO…
Ili kufanikiwa kwenye jambo lolote kwenye maisha, kwanza tengeneza mnyororo wa siku hatua za mafanikio, kisha kazi yako kubwa inakuwa ni kutokuvunja mnyororo huo.

Kama kuna tabia mpya unataka kujijengea, ifanye tabia hiyo leo, halafu ifanye kila siku, lengo lako ni isipite siku hujafanya tabia hiyo.
Mfano kuamka mapema asubuhi kila siku, kuandika kila siku, kujifunza, kufanya mazoezi n.k

Pia kama kuna tabia mbaya unataka kuivunja kwenye maisha yako, hakikisha leo hufanyi tabia hiyo, kisha baada ya hapo hakikisha kila siku huifanyi. Na wala huna haja ya kuangalia miaka mingi ijayo, wewe angalia kila siku yako mpya, na hapo jiambie utafanya nini na nini hutafanya.
Siku hiyo ikiisha ukiwa umefanya ulichopanga kufanya au kutofanya ulichopanga kutofan basi ni siku ya mafanikio makubwa kwako.

Na ili kwenda vizuri na hili, unahitaji kuweka kumbukumbu ya kukuonesha mnyororo ambayo umeshatengeneza ili usiuvunje.
Moja ya njia hizo ni kuwa na kalenda ambayo kila siku ambayo umekamilisha ulichopanga basi unaweka alama ya vyema. Sasa unapozidi kwenda utaona mfululizo wa alama za vema na hapo utajua umetengeneza mnyororo, kinachofuata ni kuepuka kuvunja mnyororo huo.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya vyovyote iwezekanavyo ili usivunje mnyororo wa tabia unayotaka kujenga au kubomoq.
#MafanikioNiNamnaUnavyoiishiSikuMoja, #TengenezaMnyororoWaMafanikioYako, #Usivunje mnyororo

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha