“But what is philosophy? Doesn’t it simply mean preparing ourselves for what may come? Don’t you understand that really amounts to saying that if I would so prepare myself to endure, then let anything happen that will? Otherwise, it would be like the boxer exiting the ring because he took some punches. Actually, you can leave the boxing ring without consequence, but what advantage would come from abandoning the pursuit of wisdom? So, what should each of us say to every trial we face? This is what I’ve trained for, for this my discipline!”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.10.6–7
Ni bahati iliyoje kwetu sisi kuiona siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Siyo kwa nguvu wala akili zetu, na wala siyo kwa sababu tunastahili zaidi ya wengine.
Ila tumeiona siku hii nyingine mpya kwa sababu bado kazi yetu haijaisha hapa duniani.
Hivyo tutumie muda wa leo vizuri kufanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwetu na kuachana na yasiyo muhimu.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAISHA YANAPOKUPIGA MAKONDE…
Falsafs inatuandaa kwa maisha kama ambavyo bondia anajiandaa kwa pambano.
Hakuna bondia anayeingia kwenye pambano akitegemea kutoka bila ya kupigwa makonde/ngumi na mwenzake.
Na hakuna bondia ambaye anaondoka ulingoni pale tu anapopokea konde kutoka kwa mwenzake.
Hiyo ni sehemu ya mchezo na anaendelea licha ya kupata makonde.
Na kadiri anavyovumilia ndivyo anavyoibuka mshindi.
Hivi ndivyo unavyopaswa kuyaendesha maisha yako,
Pale unapokutana na changamoto au magumu kwenye maisha, ni sawa na bondia anapopokea konde.
Usikimbie ulingo kwa kukata tamaa na kuona huwezi kupata unachotaka au kufika unakotaka kufika.
Chukulia magumu na changamoto unazopitia kama sehemu ya maisha,
Chukulia magumu hayo kama majaribu kwa ukomavu wako wa kifalsafa, kiimani na kimisimamo.
Endelea na safari yako ya maisha licha ya changamoto unazokutana nazo, na hapo utaweza kuibuka mshindi.
Hivi ndivyo washindi wote wanavyopatikana, kwa kuendelea na mapambano na siyo kww kukimbia.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuendelea na mipango na mikakati yako ya maisha licha ya kukutana na ugumu au changamoto.
#MafanikioSiyoRahisi, #UtaangukaSanaKablaHujawezaKusimama, #PambanaMpakaToneLaMwisho
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha