“You get what you deserve. Instead of being a good person today, you choose instead to become one tomorrow.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.22
“I don’t complain about the lack of time . . . what little I have will go far enough. Today—this day—will achieve what no tomorrow will fail to speak about. I will lay siege to the gods and shake up the world.”
—SENECA, MEDEA, 423–425

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari LEO NI LEO…
Kila mtu anajua ni kitu gani sahihi cha kufanya kwenye maisha yake,
Lakini tumekuwa tunajidanganya kwamba tutafanya kesho.
Unajua kabisa kwamba unapaswa kula kwa afya na kufanya mazoezi, lakini unajiambia utaanza kesho.
Unajua kabisa kwamba unapaswa kuwa na akiba kutoka kwenye kipato chako, lakini unajiambia utaanza kesho.
Unajua kuna kitabu au blog au makala unataka kuandika, lakini ni rahisi kujiambia utafanya kesho.

Kwa bahati mbaya sana kesho imekuwa haifiki.
Kesho imekuwa siku ya mbali sana kwa wengi, kesho ikifika unabadilika na kusema kesho tena.

Rafiki, imetosha sasa kujidanganya, imetosha sasa kujificha kwenye kivuli cha kesho.
Jiambie LEO NI LEO, kwamba chochote unachojua ni sahihi ma muhimu kufanya basi utaanza kukifanya leo.
Jiambie kabisa nitafanya leo au sitafanya kabisa.
Na kuwa wazi kwako mwenyewe pale unapojiambia kesho, jiambie tu wazi kwamba hutaki kufanya, au hufanyi ila unasingizia kesho.

Leo ni leo rafiki, kama hutafanya leo basi jua hutafanya kabisa. Kesho ni siku ya mbali sana na huwa haifiki.
Na ni nani amekupa mkataba kwamba kila kesho unayoipangia itakuja kama unavyotaka?
Unayo leo tu, itumie hiyo na acha kujidanganya na kesho ambayo hujui itakujaje.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuitumia LEO, leo hii hii na kuacha kuitegemea kesho.
#LeoNiLeo, #KeshoHaipo, #UsiahirisheYaliyoMuhimu

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha