Angalia kitu chochote kinachoanguka kwenye maisha yako, chochote ambacho kinashindwa na utaona wazi kwamba kuna mahali ulipuuza.
Kuna wakati ulipuuza kuchukua hatua muhimu ambazo ulipaswa kuchukua.
Kuna wakati ulizembea na kuchelewa kuchuka hatua ulizopaswa kuwa umechukua.
Iwe ni kazi inaaguka, labda huipendi kazi hiyo, kipato ni kidogo au umefukuzwa, ukiangalia kwa undani kuna mahali utaona wazi kwamba ulizembea au kupuuza vitu fulani.
Iwe ni kwenye biashara ambayo inaanguka, biashara ambayo haikui au inakufa, utaona zipo hatua ambazo ulizembea au kupuuza.
Na haya kwenye maisha yetu ya kila siku, kwenye afya zetu na kwenye mahusiano yetu, kama kuna chochote ambacho hakiendi vizuri, chunguza vizuri na utagundua kuna mahali ulipuuza kitu muhimu ulichopaswa kuzingatia.
Kwa kujua hili basi, kunatusaidia kuzuia vile tunavyojali visianguke, kwa kuweka umakini wetu wote kwenye vitu hivyo na kutokuruhusu uzembe wowote kuingia kwenye vile tunavyojali. Kwa kutoruhusu kupuuzia vitu kuingie kwenye yale muhimu kwetu, tutaweza kuimarisha yale ambayo ni muhimu zaidi kwetu.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,