“I’m constantly amazed by how easily we love ourselves above all others, yet we put more stock in the opinions of others than in our own estimation of self. . . . How much credence we give to the opinions our peers have of us and how little to our very own!”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 12.4
Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAONI YA WENGINE YASIKUSUMBUE…
Hakuna mtu asiyejipenda yeye mwenyewe,
Lakini cha kushangaza, huwa tunayathamini maoni ya wengine kuliko maoni yetu binafsi.
Kuna kitu umekiona na kukipenda na kukigharamia, halafu wengine wanakuambia siyo kizuri na wewe unakata tamaa.
Unajua ni namna gani unataka maisha yako yaende, unajua kipi muhimu zaidi kwako ili kuwa na maisha unayotaka. Lakini wengine wanapokuambia maisha unayotaka siyo mazuri au hayana maana basi unaachana nayo na kufanya kile ambacho kila mtu anafanya.
Rafiki, unapaswa kujikumbusha kwamba kila mtu ana maoni yake,
Na maoni ni maoni, siyo sheria.
Hivyo heshimu maoni yako kama unavyojiheshimu mwenyewe.
Na jua kila mtu ana maoni yake ambayo hayawezi kufanana na yako.
Hivyo muhimu zaidi ni kuyapa maoni yako kipaumbele.
Unajua nini unataka kwenye maisha yako, unajua kipi muhimu zaidi kwako na unajua kipi sahihi kwako kufanya. Huu ndiyo unapaswa kuwa mwongozo wako mkuu na siyo maoni ya wengine.
Usiendeshe maisha yako kwa maoni ua wengine, usifanye maamuzi makubwa kwenye maisha yako kwa sababu ya maoni ya wengine.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutokujali sana kuhusu maoni ya wengine na kuyapa maoni yako kipaumbele.
#HeshimuMaoniYako #MaoniSiyoSheria #KilaMtuAnaMaoniYake
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha