“The first thing to do—don’t get worked up. For everything happens according to the nature of all things, and in a short time you’ll be nobody and nowhere, even as the great emperors Hadrian and Augustus are now. The next thing to do—consider carefully the task at hand for what it is, while remembering that your purpose is to be a good human being. Get straight to doing what nature requires of you, and speak as you see most just and fitting—with kindness, modesty, and sincerity.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.5

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine mpya na nzuri sana tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari VITU VIWILI VYA KUZINGATIA KABLA HUJACHUKUA HATUA YOYOTE…
Matatizo na changamoto nyingi tunazokutana nazo kwenye maisha yetu, tumekuwa tunatengeneza sisi wenyewe.
Tumekuwa tunatengeneza matatizo na changamoto hizi kwa sababu tunachukua hatua kwa kusukumwa na hisia badala ya kufikiri kwa kina na kutumia misingi sahihi.

Ili kuondokana na matatizo na changamoto hizi nyingi, kuna mambo mawili muhimu sana unayopaswa kuyazingatia.
👉🏼Moja; usiumizwe na mambo yaliyo nje ya uwezo wako. Kama kuna kitu ambacho kimetokea na kipo nje ya uwezo wako, usiruhusu kikusumbue kabisa. Mfano ulipanga kufanya kitu fulani, halafu mvua kubwa ikanyesha na kukuzuia usiweze kukifanya, hata usumbuke kiasi gani, huna uwezo wa kupanga mvua inyeshe au isinyeshe. Badala yake angalia kipi unachoweza kufanya kwenye hali hiyo.

👉🏼Mbili; fanya kilicho sahihi mara zote. Kumbuka jukumu lako kubwa ni kuwa binadamu, na ubinadamu ni kufanya kile kilicho sahihi mara zote, iwe kuna watu wanaona au hakuna.
Kuwa mwema, kuwa na adabu na kuwa muwazi, hivi vitakuwezesha kufanya kilicho sahihi na utaondokana na changamoto nyingi unazopitia sasa.

Zingatia haya nawili rafiki na kila siku yako itakuwa bora sana, hutavurugwa na chochote na utafanya kilicho sahihi kila wakati.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutovurugwa na chochote na kufanya kilicho sahihi.
#UsisumbueNaYaliyoNjeYaUwezoWako, #FanyaKilichoSahihi, #FikiriKablaYaKutenda

Rafiki yako,
Makirita 3.1
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1