“I can’t call a person a hard worker just because I hear they read and write, even if working at it all night. Until I know what a person is working for, I can’t deem them industrious. . . . I can if the end they work for is their own ruling principle, having it be and remain in constant harmony with Nature.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 4.4.41; 43
Ni siku nyingine nzuri, siku mpya na ya kipekee sana kwetu wanamafanikio.
Ni nafasi bora sana kwa kila mmoja wetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo mazuri.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KABLA HUJAJISIFU WEWE NI MCHAPA KAZI…
Watu wengi hupenda kujiita wachapa kazi kwa sababu wanafanya kazi zao kwa muda mrefu.
Kwa kufanya kazi muda wote, na usiku na mchana, wengi hujiona ni wachapa kazi wakubwa.
Lakini huwezi kupima uchapa kazi kwa kigezo cha muda uliotumia, badala yake unapaswa kupima uchapa kazi wako kwa matokeo unayozalisha.
Hata kama unakesha usiku na mchana kufanya kazi, kama hakuna matokeo mazuri unayozalisha wewe siyo mchapa kazi.
Ili kupima uchapa kazi wako pamoja na umuhimu wa kile unachofanya, kuna maswali matatu muhimu sana unayopaswa kuyajibu.
Swali la kwanza ni NINI unafanya, lazima ujue kwa hakika nini unachofanya.
Swali la pili ni KWA NINI unafanya hicho unachofanya, lazima uwe na msukumo sahihi kwenye hicho unachofanya.
Swali la tatu ni WAPI matokeo ya hicho unachofanya yanakufikisha, lazima matokeo unayopata yakuwezeshe kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
Kabla hujaanza kufanya chochote, jiulize na kujipa majibu ya maswali hayo matatu.
Na kama hupati majibu, au majibu hayakuridhishi basi jua kufanya kitu hicho ni kupoteza tu muda wako. Hata ungekifanya usiku na mchana, haikufanyi kuwa mchapa kazi, sana sana inakufanya uwe mtu uliyechoka na kuvurugwa na maisha.
Jua nini unafanya, kwa nini unafanya na matokeo unayopata yanakupeleka wapi. Na kama huwezi kujibu maswali hayo matatu, ni afadhali ukalala kuliko kupoteza muda wako kufanya usichokuwa na majibu yake.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujihoji na kujipa majibu sahihi kwa kila unachofanya, ili kazi unayoweka iwe na tija.
#JuaUnachofanya, #KuwaNaMsukumoMkubwa, #ZalishaMatokeoBora
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Makirita 3.1
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1