Mafanikio kwenye maisha yetu ni sawa na ujenzi wa ghorofa, vinaendana kwa kila kitu.
Kwanza kabisa msingi lazima uwe imara, kadiri jengo linavyotegemewa kuwa refu, ndivyo msingi unavyokwenda chini na kuwa imara zaidi. Msingi wa jengo la ghorofa tano hauwezi kulingana na msingi wa jengo la ghorofa 20.
Hivyo chagua ukubwa wa mafanikio yako, kisha jenga msingi imara unaoweza kubeba mafanikio hayo. Kama msingi siyo imara, mafanikio utakayoyapata hayatadumu, yataporomoka kama ghorofa lisilo na msingi imara.
Kitu cha pili kwenye ujenzi wa ghorofa ni kitu kinachokwenda kwa hatua. Hata uwe na rasilimali nyingi kiasi gani, hutaweza kujenga jengo la ghorofa ndani ya siku moja na kukamilika. Ujenzi unahitaji muda, msingi unahitaji muda kuimarika, nguzo zinahitaji muda kuimarika.
Kwenye mafanikio yako jipe muda, usitake kupata kila kitu haraka, kuchelewa kwa vitu ni hatua ya wewe kukomaa, kuwa tayari kuvitumia vizuri pale unapovipata.
Kitu cha tatu kwenye ujenzi wa ghorofa ni kutokusumbuka na vitu vidogo vidogo. Mhandisi anapofanyia kazi mchoro wa ghorofa na kuanza ujenzi, haanzi kujiuliza ni taa za aina gani zitawekwa kwenye jengo hilo. Hilo ni jambo muhimu, lakini halimsumbui mhandisi mwanzoni mwa mradi, ni kitu ambacho maamuzi yake yatafanyika wakati utakapofika.
Kwenye mafanikio yako usikubali kusumbuliwa na mambo madogo madogo, jua wapi unakotaka kufika, jua hatua sahihi kuchukua na kisha chukua hatua hizo. Mambo mengine madogo madogo utayafanyia maamuzi wakati wake unapofika.
Jenga ghorofa yako ya mafanikio kwa kuzingatia misingi sahihi na safari yako haitakuwa nguvu kama wengi wanavyozifanya safari zao za mafanikio kuwa ngumu.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Msingi ndiyo kila
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha nihangaike na kujenga msingi imara kisha mambo mengine madogo madogo nitakutana nayo mbele. Nisihangaike saana na ni taa gani nitaziweka lilio muhimu kwasasa ni kuhakikisha kuwa jengo imara linasimama.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike