“Don’t you know life is like a military campaign? One must serve on watch, another in reconnaissance, another on the front line. . . . So it is for us—each person’s life is a kind of battle, and a long and varied one too. You must keep watch like a soldier and do everything commanded. . . . You have been stationed in a key post, not some lowly place, and not for a short time but for life.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.24.31–36

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Tumepata nafasi nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MAISHA NI UWANJA WA MAPAMBANO…
Maisha yetu ni vita,
Na kila siku tuko kwenye mapambano ili kuendelea kuwa hai ma hata kufanikiwa kwenye maisha yetu.
Mapambano haya siyo lele mama, yanahitaji kujitoa kweli ili kuweza kushinda vita hii.

Unapambana na matrilioni ya viumbe hai wengine ambao wananufaika kupitia mwili wako.
Unapambana na wewe mwenyewe, kwa tabia zako ambazo zinakurudisha nyuma.
Unapambana na mazingira na hali ambazo siyo rafiki kwako kwa malengo na mipango uliyonayo.
Unapambana na watu wengine ambao wanakukatisha tamaa au wanashindana na wewe.

Hakuna wakati ambapo vita hii inakuwa rahisi, kila siku ni siku ya mapambano na kila siku unapaswa kuwa imara zaidi.
Unapaswa kuwa mpambanaji shupavu ili kuweza kushinda vita hii, ambayo ni vita ya maisha.
Tangu umezaliwa mpaka siku utakayokufa, kila siku itakuwa siku ya mapambano.

Sifa zitakazokuwezesha kushinda vita hii ni UJASIRI, NIDHAMU, KUJUA UNACHOTAKA, KUTOKUWA MBINAFSI, KUJITOA, na KUJIPANGA VIZURI.
Sifa zitakazofanya ushindwe vita hii ni WOGA, PAPARA, UBINAFSI, KUTOKUJIPANGA, KUJIAMINI KUPITA KIASI na WOGA.
Nina imani kubwa juu yako kwamba utashinda vita hii.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kupambana ili kuweza kushinda kwenye vita hii ya maisha.
#MaishaNiVita, #PambanaMpakaToneLaMwisho #SimamiaMisingiSahihi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1