“How does it help, my husband, to make misfortune heavier by complaining about it? This is more fit for a king—to seize your adversities head on. The more precarious his situation, the more imminent his fall from power, the more firmly he should be resolved to stand and fight. It isn’t manly to retreat from fortune.”
—SENECA, OEDIPUS, 80

Ni furaha iliyoje kwetu sisi kuweza kuiona siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Siyo wote waliolala jana wamepata nafasi hii, hivyo ni bahati kubwa kwetu.
Na njia pekee ya kutumia bahati hii ni kwa kushukuru na kisha kutumia muda wetu na nguvu zetu vizuri, kwa yale ambayo ni muhimu zaidi.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UGUMU UNADHIHIRISHA…
Mambo yanapokuwa mazuri, watu wanaweza kuigiza kwa namna wanavyotaka.
Ni pale mambo yanapokuwa magumu ndipo ukweli wote unapojidhihirisha.
Magumu yanadhihirisha ukweli kuhusu mtu na hali pia.
Pale mambo yanapokuwa mazuri na rahisi, kila mtu anaweza kuonekana yuko vizuri, ni mpaka mambo yanapobadilika na kuwa magumu ndiyo tunajua nani hasa yuko vizuri.
Pale ambapo hakuna ugumu wala majaribu, kila mtu anaweza kusema anaishi misingi fulani, ni mpaka pale magumu na majaribu yanamtikisa mtu mpaka anaachana na misingi anayowaambia watu anaiishi.

Bilionea Mwekezaji Warren Buffett anasema mawimbi yanapotulia ndiyo tunajua nani anaogelea uchi. Ukitumia mfano wa uwekezaji kwamba pale uchumi unapokuwa vizuri, kila mtu anajiita mwekezaji bora, kwa faida rahisi inayopatikana. Lakini uchumi unapobadilika na kuwa mgumu, hapo ndipo wengi hupotea na kubaki wale wawekezaji wa kweli.

Unapokutana na magumu kwenye maisha yako, jua huo ndiyo wakati wa kudhihirisha kile ambacho kipo ndani yako kweli.
Hivyo unapopitia magumu, simama imara, usikubali kutetereka, usikubali kurudi nyuma.
Kwa sababu kama utakuwa imara kwenye magumu, hakuna chochote kitakachoweza kukuzuia kufanikiwa.

Naamini kwa maarifa unayopata na hatua unazochukua wewe siyo mmoja wa waigizaji au wale wanaoogelea uchi na kufichwa na mawimbi.
Kazana kuwa wewe, kazana kuwa imara na simamia misingi yako kila wakati, hasa nyakati ngumu.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kudhihirisha uimara wako pale unapokutana na magumu.
#MafanikioHayaigizwi #MagumuNiKipimo #KazanaKuwaBoraKilaWakati

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1