Mpendwa rafiki yangu,

Mamilioni ya watu waliona maembe yakianguka chini,lakini mwanasayansi Newton tu ndiye aliyewahi kuuliza kwanini.  Mara nyingi katika maisha yetu vingi vinatokea lakini hatujawahi kujiuliza kwanini vitu vinakwenda hivi. Wewe mwenyewe umeshawahi kujiuliza kwanini embe huwa linadondoka chini lenyewe?

Sifa ya kwanini ni sifa ambayo kila kiongozi anapaswa kuwa nayo kwenye uongozi wake. Ninaposema kiongozi namaanisha kila mtu kwa sababu hata kama wewe huwaongozi wengine unajiongoza wewe mwenyewe. Kiongozi unatakiwa kuwa na kwanini, kwanini itakusaidia kubaini mambo mengi. Usipokuwa mtu wa kuhoji mambo vizuri basi unakosa sifa ya kiongozi, kila kiongozi anatakiwa kuhoji na siyo kupokea mambo kama yalivyo.

breakthrough

Uongozi ni kufungua thamani za watu zilizopo ndani yao na kuwafanya kuwa bora.  Kiongozi ni kuwaonesha wengine njia ya kupita na sivyo vinginevyo.

Ipi ndiyo namna bora ya kuongoza watu?

Don Shula aliwahi kusema sijui namna nyin ya kuongoza lakini ni kwa mfano. Hivyo basi, namna bora ya kuongoza ni kwa mfano. Watu wanapenda sana kuongozwa kwa mifano, kile unachokileta kwa wale unaowaongoza ingekuwa vema na wewe unaweza kukifanya au umeshakifanya tayari.

Watu wanahamasika sana pale wanapomuona na kiongozi wao ndiyo mfano wa kufanya kile anachowaamuru kufanya. Ukiwa ni kiongozi wa imla yaani wewe ni kusema tu lakini hujitoi kwa mifano, siyo njia bora ya kuongoza watu. Watu hawatahamasika  kwa kwenda kinyume na kanuni za uongozi.

Unapokuwa kiongozi basi, usitumie uongozi wako vibaya kuwaumiza watu, bali tumia uongozi wako kuwainua watu. Wape watu faraja, matumaini ya kuona mbele na siyo kuwakatisha tamaa.

SOMA;Hii Ndiyo Nguzo Muhimu Kwa Kiongozi Yoyote Yule

Waaminishe wale unaowaongoza kuwa maisha yanawezekana endapo mtu akiamua kuchukua kuwa jukumu la maisha yake ni lake mwenyewe na siyo la kiongozi. Wako watu wanafikiria kuwa jukumu la maisha yao siyo lao bali ni la kiongozi kitu kama hiko kinawafanya viongozi wengi kupata lawama ambazo hawazistahili kuzibeba.

Hatua ya kuchukua leo; kwa kiongozi yeyote au yule ambaye siyo kiongozi wa kundi kubwa la watu lakini ni kiongozi hakikisha unakuwa na namna bora ya uongozi ambao ni kuongoza kwa mfano.

Hivyo basi, licha ya kuwa na kiongozi ambaye anakuwa anatupa dira, ila usikae chini na kujisahau kuwa yeye ndiyo anahusika na  wewe kila kitu. kumbuka hakuna kiongozi anayekosa usingizi kwa ajili yako, maisha ni yako pambana kila siku kuwa bora.

Makala hii imeandikwa na

Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa www.mtaalamu.net/kessydeo, vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI.  Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana