“Never shirk the proper dispatch of your duty, no matter if you are freezing or hot, groggy or well-rested, vilified or praised, not even if dying or pressed by other demands. Even dying is one of the important assignments of life and, in this as in all else, make the most of your resources to do well the duty at hand.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.2
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ambayo tumeiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari TEKELEZA MAJUKUMU YAKO…
Tofauti ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa haipo kwenye kuweka malengo au mipango.
Bali ipo kwenye utekelezaji wa ile mipango ambayo mtu amejiwekea.
Wanaofanikiwa sana ni wale ambao wanatekeleza mipango waliyojiwekea na wanafanya hivyo bila ya kuruhusu sababu yoyote kuwazuia.
Watu hawa wanafanya walichopanga kufanya iwe wanajisikia au hawajisikii, iwe kuna mvua au kuna jua.
Kwao, wakishapanga wanafanya, hakuna tena mjadala hapo.
Tatizo kubwa lipo kwa wale wanaoshindwa, wale ambao hawapigi hatua kubwa kwenye maisha yao.
Watu hawa ni wazuri sana kwenye kupanga,
Lakini inapokuja kwenye kuchukua hatua, huwa wanatafuta kila aina ya sababu kwa nini waahirishe kile walichopanga.
Hivyo ikijitokeza sababu yoyote ile, hata kama siyo ya msingi, basi inawatosha kuacha kutekeleza kile walichopanga.
Watu hawa hufanya kitu pale wanapojisikia, wasipojisikia hawafanyi.
Watu hawa husubiri mpaka kila kitu kikae sawa ndiyo wafanye, kama kuna kitu kinakosekana basi hutumia kama sababu ya kutokufanya.
Rafiki, kama unataka kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako, basi kuwa mtu wa kutekeleza majukumu yako.
Fanya kile ulichopanga kufanya na usiruhusu sababu yoyote ikuzuie kufanya.
Amua kisha fanya, iwe unajisikia au hujisikii, kuna jua au kuna mvua na wala usiangalie wengine. Wewe fanya.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutekeleza majukumu yako, kufanya ulichopanga kufanya bila ya kuruhusu sababu yoyote kukuzuia.
#FanyaUlichopanga #UsitafuteSababu #UsijitorokeMwenyewe
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1