“As you move forward along the path of reason, people will stand in your way. They will never be able to keep you from doing what’s sound, so don’t let them knock out your goodwill for them. Keep a steady watch on both fronts, not only for well-based judgments and actions, but also for gentleness with those who would obstruct our path or create other difficulties. For getting angry is also a weakness, just as much as abandoning the task or surrendering under panic. For doing either is an equal desertion—the one by shrinking back and the other by estrangement from family and friend.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 11.9
Chukua dakika moja ya kukaa kimya na kushukuru kwa siku hii nyingine mpya ambayo umeipata,
Siyo kwa nguvu zako waka akili yako, bali ni bahati tu kwako kuiona siku hii.
Wapo ambao wangekuwa tayari kulipa mamilioni ya fedha ili tu waione siku hii, lakini hawajapata bahati uliyoipata wewe.
Hivyo kitu sahihi kwako kufanya ni kushukuru na kisha kuitumia siku hii vyema, kwa kuhakikisha hupotezi hata dakika moja kwa mambo yasiyo muhimu.
Leo hii nenda kaishi kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA na utaweza kufanya nakubwa sana leo na kila siku ya maisha yako.
Asubuhi hii tutafakari USIIACHE NJIA SAHIHI KWA SABABU YA WENGINE…
Utakapochagua kuyaishi maisha ya mafanikio, utakapochagua kuiishi misingi ya mafanikio, wataibuka watu wa kila aina na kuleta vikwazo kwako.
Chagua kujituma sana kwenye kazi zako na watakuambia unapaswa kuwa na maisha ya mlinganyo, fanya kazi muda kidogo na upate mapunziko.
Chagua kudhibiti matumizi yako na watakuambia ni bahili, unajitesa na una roho mbaya, hasa kama huwapi watu fedha kama wanavyotaka wao.
Chagua kula kwa afya na watakuambia unajitesa au utakufa tu, usijisumbue.
Rafiki, kwa vile watu wanaotuambia hivi ni wa karibu kabisa kwetu, na wanarudia rudia kutuambia mara kwa mara, ni rahisi kushawishika, kuacha yake maisha uliyochagua na kuishi kama wanavyokuambia wao.
Na hapo ndipo unakuwa umetangaza kushindwa na kuachana kabisa na mafanikio.
Rafiki, kitu sahihi kwako kufanya siyo kile ambacho wengine wanakuambua ni sahihi kufanya, bali kile unachojua wewe ni sahihi kufanya kwa hali uliyonayo sasa.
Mfano kama bado hujafikia uhuru wa kifedha, huna anasa ya kufanya kazi kwa muda mfupi au kuwa na siku za mapumziko. Hivyo kufanya kazi masaa 16 lwa siku na siku zote saba za wiki ni kitu sahihi kwako.
Lakini utakapoanza kufanya hivyo, wataibuka watu na kukuambia unapaswa ufanye kazi masaa 8 tu kwa siku na siku 6 kwa wiki, ya saba upumzike. Ukiwasikiliza na kuwafuata, unaishia kuwa kama wao.
Hivyo rafiki, usiiache njia sahihi kwako kwa sababu ya wengine, simamia kile kilicho sahihi.
Lakini pia usiwaache kabisa wengine kwa sababu ya njia yako sahihi. Bali hakikisha mambo yao hayaathiri njia uliyochagua.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuichagua njia sahihi kwako na kuifuata bila ya kujali wengine wanasemaje.
#FanyaKilichoSahihi #UsiweKawaida #UsiyumbishweNaMaoniYaWengine
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1