“The unjust person acts against the gods. For insofar as the nature of the universe made rational creatures for the sake of each other, with an eye toward mutual benefit based on true value and never for harm, anyone breaking nature’s will obviously acts against the oldest of gods.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 9.1.1

Hongera sana mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana kwetu leo.
Ni fursa bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari SIMAMIA HAKI…
Mafanikio yetu hapa duniani ni matokeo ya namna tulivyowawezesha wengine kufanikiwa zaidi.
Mwalimu anafanikiwa kama wanafunzi wake wanafanikiwa.
Daktari anafanikiwa kama wagonjwa wake wanapona.
Wenye viwanda wanafanikiwa kama bidhaa wanazotengeneza zinawafanya watu wafanikiwe zaidi.
Waliofanikiwa wanafanikiwa pale waliowaajjri wanapofanikiwa zaidi.
Na biashara zinafanikiwa pale ambapo wateja wa biashara hizo wanafanikiwa zaidi.

Hakuna mafanikio yanayokuja kwa kujiangalia na kujifikiria sisi wenyewe pekee.
Mafanikio yetu yapo kwa watu wengine.
Hivyo basi, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwa msimamizi wa haki, wa kufanya kile kilicho sahihi mara zote, kufanya kile chenye manufaa kwa wengine.
Ni kwa kusimamia haki ndiyo tunaweza kuwajali zaidi wengine, wakafanikiwa na sisi tukafanikiwa zaidi.
Lakini kama tutajiangalia sisi wenyewe pekee, tutashindwa kufanikiwa na tutaharibu sana mahusiano yetu na wengine.

Marcus Aurelius anatuambia kama kitu siyo kizuri kwa asali, basi siyo kizuri kwa nyuki.
Na Immanuel Kant anatuambia mara zote jiulize kama kila mtu duniani angefanya kama unavyofanya wewe, je dunia itakuwa nzuri na salama? Kama jibu ni hapana usifanye.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kusimamia haki na kufanya kile chenye manufaa kwa wengine.
#SimamiaHaki #FanyaKilichoSahihi #JaliMaslahiYaWengine

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1