“Nothing is noble if it’s done unwillingly or under compulsion. Every noble deed is voluntary.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 66.16b

Tuchukue nafasi hii kushukuru kwa bahati hii tuliyoipata ya kuiona siku hii mpya na ya kipekee sana kwetu.
Wote tunajua hii ni bahati tu, siyo nguvu zetu waka ujanja wetu.
Hivyo tunapaswa kujikumbusha hili siku nzima ya leo, hasa pale tunapokuwa tunapoteza muda wetu kwa vitu ambavyo siyo muhimu.
Jiulize, je kama leo ingekuwa ndiyo siku yako ya mwishi hapa duniani, ungetumia muda wako kufanya vile unavyosumbuka navyo sasa?
Kama jibu ni hapana basi acha mara moja, siyo muhimu na haina manufaa kwako.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NI HIARI YAKO…
Hakuna jambo jema linaloweza kufanywa kwa kulazimishwa.
Pamoja na sheria na taratibu mbalimbali za kuwabana watu wasifanye maovu, bado maovu yanaendelea kufanyika kila siku.
Pamoja na dini kuwa na amri kali zinazozuia watu wasiende kinyume na taratibu za dini hizo, bado wengi wanakwenda kinyume.
Wakiwa hadharani wanafanya kile ambacho utaratibu unawataka wafanye, wakiwa faraghani wanafanya kinyume.

Hii ina maana kwamba, kufanya kile kilicho sahihi, iwe upo hadharabi au faraghani ni hiari yako mwenyewe. Ni wewe pekee unayeweza kuchagua kufanya kilicho sahihi na kuwa na maisha bora.
Hakuna anayeweza kukulazimisha au kukushurutisha.

Hivyo wito wangu kwako leo rafiki yangu ni kifanya maamuzi yako mwenyewe, kuchagua kufanya kikicho sahihi, kwa sababu umechagua kufanya na siyo kwa sababu umelazimishwa kufanya.
Unapochagua kufanye mwenyewe, inakuwa na maana kubwa zaidi kwako kuliko ukilazimishwa kufanya.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchagua kwa hiari yako kufanya kile kilicho sahihi kwako na wengine pia.
#NiHiariYako #FanyaKilichoSahihi #MaishaNiKuchagua

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1