“Some people are sharp and others dull; some are raised in a better environment, others in worse, the latter, having inferior habits and nurture, will require more by way of proof and careful instruction to master these teachings and to be formed by them—in the same way that bodies in a bad state must be given a great deal of care when perfect health is sought.”
—MUSONIUS RUFUS, LECTURES, 1.1.33–1.3.1–3.

Shukrani ndiyo kitu pekee cha kutoa kwa sisi kuiona siku hii nyingine nzuri ya leo.
Siyo kwa nguvu zetu wala akili zetu, bali ni kwa neema tu ndiyo tumeweza kuiona siku hii bora ya leo.
Kuitumia siku hii vizuri ndiyo namna pekee ya kuweza kunufaika nayo na kuwanufaisha wengine pia.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari BAHATI INAHUSIKA…
Kila mmoja wetu, kuna bahati ambayo amewahi kukutana nayo au kupitia kwenye maisha yake.
Huenda umezaliwa na kipaji fulani ambacho wengine hawana,
Huenda umekulia mazingira yaliyokujenga vizuri kuliko wengine,
Huenda umekutana na fursa ambazo ni bora zaidi kwako,
Huenda umekutana na magumu, ambayo yalikusukuma ukawa bora kuliko ulivyokuwa awali.
Hizo zote ni bahati na kila mmoja wetu kuna bahati anayo, kitu fulani ambacho yeye anacho na wengine hawana.

Hivyo tunatumiaje bahati zetu?
Moja kwa kutambua kwamba kuna maeneo tuna bahati na kutumia bahati hizo vizuri.
Kuacha kuangalia tumekosa nini na kuangalia kile cha tofauti tulichonacho na kukitumia vizuri.
Kuna kipaji unacho basi kitumie vizuri, kuna fursa umeipata basi itumie vyema.
Kwa kuangalia kile ulichonacho na kukitumia vizuri, hutapata muda wa kuangalia umekosa nini.

Upande wa pili ni kuwaelewa wale ambao hawapo kama wewe,
Usimdharau mtu kwa sababu hawezi kufanya kama wewe au hajafika pale ulipofika wewe.
Huenda hajakutana na bahati ambazo umekutana nazo wewe.
Hajapitia yale uliyopitia wewe na hana kile kilichopo ndani yako.
Hivyo unapojihusisha na wengine, waelewe na wavumilie pale ambapo hawapo kama ulivyo au unavyotaka wewe.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujua bahati ulizonazo na jinsi ya kuzitumia kuwa bora zaidi na kuwanufaisha wengine pia, pamoja na kuwaelewa wale ambao hawajapata bahati ulizopata wewe.
#BahatiInahusika #UnaKituChaTofauti #WaeleweWengine

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1