“Trust me, real joy is a serious thing. Do you think someone can, in the charming expression, blithely dismiss death with an easy disposition? Or swing open the door to poverty, keep pleasures in check, or meditate on the endurance of suffering? The one who is comfortable with turning these thoughts over is truly full of joy, but hardly cheerful. It’s exactly such a joy that I would wish for you to possess, for it will never run dry once you’ve laid claim to its source.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 23.4

Ni siku mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari FURAHA YA USTOA…
Watu wengi wamekuwa hawana furaha kwenye maisha kwa sababu wanajipa masharti ya kuwa na furaha.
Wengi hujiambia nikishapata kitu fulani basi nitakuwa na furaha.
Wanaweza kupata kweli kitu hicho, lakini wasiwe na furaha, au wakiwa nayo isidumu.

Kwenye Falsafa ya Ustoa, furaha ni kitu cha kudumu, ni kitu ambacho unakuwa nacho muda wote, bila ya kujali umepata au imekosa nini.
Kwa kuwa Mstoa unapaswa kufurahia unapopata na kufurahia unapopoteza,
Kufurahia mambo yanapokuwa mazuri na kufurahia mambo yanapokuwa mabaya.
Kwa sababu kila kitu kinakuja kwako kwa sababu, kuna kusudi la kila kitu, hivyo unapopokea kila kitu kwa furaha, unakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupiga hatua zaidi.

Usijiwekee masharti kwenye furaha,
Usijiwekee vigezo vya furaha,
Furaha inapaswa kuwa hali ya kudumu kwako,
Kwa kuwa inaanza na wewe na haijalishi nini kinachoendelea nje.
Ukiweza kuwa na furaha hii ya kudumu ya ustoa, utakuwa na maisha bora wakati wote.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa na furaha ya kudumu, furaha ambayo haitegemei hali ya nje.
#FurahaZaoLaNdani #UsijiwekeeMashartiYaFuraha #FurahiaKilaKinachotokea

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1