“That cucumber is bitter, so toss it out! There are thorns on the path, then keep away! Enough said. Why ponder the existence of nuisance? Such thinking would make you a laughing-stock to the true student of Nature, just as a carpenter or cobbler would laugh if you pointed out the sawdust and chips on the floors of their shops. Yet while those shopkeepers have dustbins for disposal, Nature has no need of them.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.50
Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi nyingine bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari USISUBIRI UKAMILIFU. ….
Kitu ambacho kimekuwa kinawakwamisha wengi kufanikiwa ni kusubiri ukamilifu.
Wengi hutaka kila kitu kiwe sawa na kamili ndiyo waanze.
Lakini hivyo sivyo dunia na asili inavyojiendesha.
Hakuna chochote duniani ambacho kimekamilika, lakini dunia inakwenda.
Hivyo acha kusubiria ukamilifu ndipo uanze chochote unachotaka kuanza,
Anzia pale ulipo sasa, kisha kazana kuboresha zaidi.
Kufanya chochote ni bora kuliko kutokufanya chochote kabisa.
Chochote unachojiambia bado hujawa tayari kuanza kufanya, anza kukifanya sasa na utaona fursa za kufanya kwa ubora zaidi.
Unapoanza unajifunza vitu ambavyo usingejua kama hujaanza.
Unapoanza unajiweka kwenye mwendo na hivyo kuwa rahisi zaidi kwako kuendelea na mwendo huo.
Anza sasa, usisubiri ukamilifu.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuanzia pale ulipo sasa na kutokusubiri ukamilifu.
#AnziaHapoUlipoSasa #UsisubiriUkamilifu #KufanyaChochoteNiBora
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1