“You must stop blaming God, and not blame any person. You must completely control your desire and shift your avoidance to what lies within your reasoned choice. You must no longer feel anger, resentment, envy, or regret.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.22.13

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni siku bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USILAUMU, CHUKUA HATUA…
Ni rahisi kutafuta na kupata watu wa kuwalaumu pale mambo yanapokwenda tofauti na ulivyotegemea.
Ni rahisi kuona kwamba kuna namna wengine wanakukwamisha usipige hatua.
Na hili limekuwa sababu kubwa ya wengi kukwama na kushindwa kupiga hatua.
Kwa sababu haijalishi wengine wamechangia kiasi gani kwenye mambo yako kukwama, bado una uhuru mkubwa ndani yako wa kuchagua uchukulieje kila kinachotokea kwenye maisha yako.

Ni lazima uache kumlaumu Mungu kwa kuona kama amekusahau au kwa kusema kwa nini wewe.
Ni lazima uache kulaumu mtu yeyote yule na badala yake kubeba jukumu la maisha yako.
Ni lazima udhibiti fikra na hisia zako, kwa kuweka mkazo kwenye yale unayoweza kufanya kuondoka pale ulipokwama na siyo kuangalia nani kakifikisha hapo.
Usijiruhusu kuwa na hasira, chuki, wivu au majuto kwa mtu mwingine yeyote.

Jukumu lako kubwa ni moja, kuangalia hatua gani unaweza kuchukua kwenye kila hali unayopitia na kisha chukua hatua hiyo.
Kulaumu au kulalamika ni kupoteza muda wako, haina msaada wowote kwako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuacha kabisa kulaumu wengine na kuchukua hatua kuyafanya mambo yawe bora zaidi.
#UsilaumuYeyote #ChukuaHatuaSahihi #DhibitiFikraNaHisiaZako

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1