“Wherever a person can live, there one can also live well; life is also in the demands of court, there too one can live well.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 5.16
Ni siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari POPOTE ULIPO, UNA NAFASI YA KUISHI KWA MISINGI YAKO.
Kuna wakati tunasingizia hali tunazopitia au mazingira tuliyopo kama sababu ya sisi kushindwa kuiishi misingi ambayo tumejiwekea kwenye maisha yetu.
Labda ni kazi unayofanya, ambapo wengine wote unaofanya naonkazi hiyo wanatumia njia za mkato na hawajali sana, hivyo unajiambia kila mtu anafanya, huna namna bali kufanya pia.
Au ni biashara unayofanya, ambapo wafanyabiashara wengine siyo waaminifu na wanawalaghai wateja. Unajiambia kwa kuwa kila mtu anafanya na mazingira yanachochea hilo, huna budi na wewe kufanya.
Rafiki, unapochagua kuishi kwa misingi fulani, unapaswa kuisimamia misingi hiyo kila wakati na kila mahali.
Kama tu upo hai, unayo nafasi ya kuishi kwa misingo yako.
Na kuishi kwa misingi hiyo halitakuwa zoezi rahisi,
Kuna watu watakupinga, wengine watakubeza na wengine watakuona wewe ni adui mkubwa kwao.
Lakini kamwe usikubali wakuangushe kwenye kuiishi misingi yako.
Chagua kuiishi na kuisimamia misingi yako nyakati zote na mahali popote.
Kunguka yule ambaye hana anachosimamia, basi ataangushwa na kila kitu. Chagua kusimamia misingi yako na hakuna kitakachoweza kukuangusha.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuishi na kusimamia misingi yako ya maisha bila ya kujali hali au mazingira unayokuwepo.
#SimamiaMisingi #UsiyumbishweNaChochote #KazanaKuwaBoraKilaWakati
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1