Kabla hujafikia maamuzi yoyote muhimu kwenye maisha yako, ni vyema ufanye utafiti mdogo na kuangalia namba zinasemaje.

Kwa sababu maneno yanaweza kudanganya sana, lakini namba huwa hazidanganyi, kamwe.

Mtu anakushauri ukiingia kwenye kilimo cha matikiti utapata faida sana, ukiweka milioni mbili utapata milioni kumi. Mjibu vizuri, hebu nioneshe hizo namba halisi, kwako wewe au mtu mwingine aliyelima akapata hivyo. Swali hilo tu linatosha kukupa mwanga kama unachoambiwa ni sahihi au la.

Na hapa hatuzungumzii zile namba za kwenye makaratasi, zile za kupiga hesabu za kusema tuchukulie heka moja inatoa matikiti elfu moja, na tikiti moja utauza kwa elfu moja bei ya chini… hizo siyo namba, hizo ni hadithi za kujifariji.

Namba kamili ni zile ambazo ni halisi, ambazo zinaonesha kweli kilichofanyika na siyo kinachoweza kufanyika.

Ukisimamia namba, mara zote utafanya maamuzi sahihi na hakuna anayeweza kukulaghai.

Lakini pia unapaswa kuwa makini kwenye usomaji wa namba, maana kuna wajanja wanaoweza kuzigeuza namba mbaya zikaonekana ni nzuri. Kama hujui hilo soma kitabu HOW TO LIE WITH STATISTICS, unaweza kupakua kitabu hicho hapa; http://bit.ly/kudanganyakwanamba

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha