Mpendwa rafiki yangu,

Moja ya matatizo mengi yanayoyotokea katika maeneo yetu ya maisha na watu kufanya kinyume chake ni kwa sababu ya ujinga. Ujinga ni mzigo usiobebeka, watu wengi hawapendi kujifunza na kubadilika katika maisha yao. Na watu huwa wanachoka kuona mazoea ya kila siku, hivyo usipochukua hatua ya kujiongeza utaishia kupoteza.

Katika eneo la mahusiano hususani la ndoa wanandoa wengi wanachukulia poa kuhusu kujifunza maeneo ya ndoa. Mtu anaona akishaoa au kuolewa amemaliza kazi. Hapana bado hujamaliza kazi, kupanda mbegu ardhini siyo kwamba ndiyo umemaliza kazi, bado unahitaji kuweka kazi ya kuhudumia mbegu uliyopanda iote, uimwagilie,uipalilie mpaka pale utakapofikia wakati wa kuvuna.

KAVA IJUE NJAA YA WANANDOA

Ujinga umetawala katika ndoa, kwanini? Wanandoa wanaishi kimazoea hawataki kubadilika, na moja ya sababu ambayo watu wengi huwa wanazichoka ndoa zao ni mazoea yaani hakuna kipya kila siku ni yale yale kama jana. Kama usipojiongea na kujifunza juu ya ndoa yako utapoteza ladha katika ndoa yako utakua kama chakula kisichokuwa na chumvi, si unajua chakula kisichokuwa na chumvi hakina ladha? Je uko tayari kula chakula ambacho hakina chumvi? Kama jibu lako ni hapana jifunze  basi mambo mapya katika ndoa yako ili uiboresha, vitabu vipo ni wewe tu kuchukua hatua na kusoma.

Sababu kuu moja inayosababisha ndoa nyingi kuelekea kuwa ndoa za Bluetooth ni changamoto ya kutopeana muda.

Ndoa za Bluetooth maana yake ni zile ndoa za mbali, kwa mfano,mume yuko bukoba na mke yuko arusha, unaona hapo! Ndoa za mbali zilivyo na changamoto? dhumuni la ndoa siyo kuishi mbalimbali bali kuishi kwa pamoja.

Watu wengi wanaishi katika ndoa lakini ni kama vile ndoa za Bluetooth kwa sababu wanandoa licha ya kuwa karibu kila siku lakini hawapeani muda. Na sababu kubwa ni majukumu, hivi kuwa bize kiasi kusahau ndoa yako ni salama unafikiri? Kama humpatii muda mwezi wako unafikiri nani anatakiwa kumpatia muda?

Mara nyingi watu wanachukulia poa mahusiano yao, wanaamini wakishaoa au kuolewa wamemaliza kazi, binadamu ni viumbe wa hisia hivyo wanahitaji muda, utakiwa kuwa na quality time na mwezi wako. Na dunia iko hivi, usipofanya majukumu yako vizuri itakusaidia kufanya majukumu hayo kwa riba.

Tatizo kubwa la watu kuamua kwenda nje ya ndoa huenda ni kokosa kile anachokitaka ndani ya ndoa lakini, kabla hujaenda nje ya ndoa unafikiri hilo ndiyo suluhisho?  Suluhisho ni kukaa na mwenzako na kumueleza abc ambazo anatakiwa kufanya. Mwenzi wako amekamilika ila tatizo ni wewe mwenyewe ambaye unashindwa kumtumia vizuri.

Waswahili wanasema mchele ni mmoja ila mapishi mbalimbali kama unaona mwenzako anapika pilau zuri kushinda wewe kwanini usichukue hatua ya kujifunza na wewe ulipike kwako? Kile ambacho unaona ni kizuri kwa ustawahi wa ndoa yako kifanyie kazi na siyo kukimbilia kutafuta nje na wakati uwezo wa kukileta uko ndani yako.

Ubize usiharibu ndoa yako, mwenzi wako anahitaji muda na mahusiano ni muda kama umeshindwa kumpa mwenzako muda utamwachia upweke, na ukimwacha na upweke atatafuta wa kulizipa pengo hilo.

SOMA; Kama Unataka Kuboresha Mahusiano Yako Tumia Falsafa Hii Hapa

Hatua ya kuchukua leo; Ndoa yako ni kazi kama zilivyo kazi nyingine. Kila siku jifunze ili kuwa na ndoa bora, usichukulie ni kitu simpo, bali ndoa ni kazi. Na hakuna kazi bila kuweka kazi kama unataka matokeo bora kwenye ndoa yako.

Kama unataka ndoa yako iwe bora na bado hujachukua hatua ya kusoma kitabu cha IJUE NJAA YA WANANDOA fanya malipo ya shilingi elfu 10 sasa  ya kutuma fedha kupitia namba 0717101505/0767101504 na utatumiwa kitabu chako.

Kwahiyo, jifunze kila siku kwenye eneo lako la ndoa ili uwe bora, mpe mwenzako muda na mpe kile anachotaka kwani wewe ndiyo mteja wake wa kwanza. Usipompa mteja kile anachokitaka atakwenda kukitafuta kule ambako kipo.

Makala hii imeandikwa na

Mwl. Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa  http://kessydeo.home.blog

vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI.  Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana