“Inwardly, we ought to be different in every respect, but our outward dress should blend in with the crowd.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 5.2

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii mpya na bora sana tuliyoiona leo.
Ni siku bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NJE NA NDANI…
Unaweza kuwa na misingi na misimamo yako ya maisha unayoiishi, lakini hii iweke zaidi ndani yako kuliko kutaka kujionesha kwa nje.
Hii ni kwa sababu watu hupenda kuhoji, kukosoa na kushambulia chochote ambacho ni tofauti na walivyozoea wao.

Hivyo ishi utakavyo ndani yako, lakini kwa nje, kwenye mwonekano, mavazi na vitu vingine vya juu juu, kuwa kama wengine.
Hilo litakupunguzia usumbufu wa kuhitaji kujieleza kila wakati na kwa kila mtu.
Hili ni kwa yale mambo madogo madogo ya nje kama mavazi, mwonekano na mengineyo.
Haitakwenda kinyume na msimamo na misingi yako kama utavaa kama wanavyovaa wengine.
Lakini inapokuja kwenye maadili unayoyasimamia, endelea kuyasimamia.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchagua maisha ya ndani yanayoendana na misingi yako, na maisha ya nje ambayo hayatakupa usumbufu, lakini pia yasiyovunja misingi yako.
#IshiMisingiNdani #NjeKamaWengine #MaishaSiyoMaonesho

MUHIMU; Tunaendelea na juma la KUWA NA VIPAUMBELE NA KUFANYA MACHACHE ili kuwa na muda zaidi. Leo kaendelee na zoezi la kujiuliza maswali matatu kabla hujafanya jambo, #AfyaUtajiriHekima. Kupata zawadi ya kitabu changu na cha Seneca kuhusu muda, tuma elfu 5 kwa namba 0717396253/0755953887 kisha tuma email yako na utatumiwa zawadi. Kwenye mjadala wetu wa jioni karibu utushirikishe yale uliyoepuka kufanya leo.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1