Rafiki yangu mpendwa, kwenye makala hii nakwenda kukuonesha adui mkubwa wa mafanikio yako, ambaye amekuwa anakazana sana usifanikiwe na jinsi ya kumshinda asiwe kikwazo tena kwako, na utajifunza hilo kwa mfano halisi. Karibu twende pamoja.

Kipo kichekesho kimoja kinachosema kwamba, nchini Marekani, umeme ukikatika mtu anaanza kwa kujiuliza nini kimetokea kwenye nyumba yake. Lakini nchini Tanzania umeme unapokatika, mtu anaanza kwa kutoka kwanza nje na kuangalia kama kwa wengine kuna umeme.

Ni kichekesho kidogo na kinachoonekana cha kawaida sana, lakini kina funzo kubwa sana ndani yake, funzo ambalo ukiweza kulielewa litabadili kabisa maisha yako na kuyafanya kuwa bora zaidi.

Funzo lenyewe ni hili; mara nyingi tatizo linapotokea, au tunapokutana na kikwazo kwenye maisha, huwa tunakimbilia kuangalia kwanza nje badala ya ndani. Huwa tunakimbilia kutafuta wa kuwapa lawama badala ya kubeba majukumu yetu wenyewe. Na hili limekuwa kikwazo kikubwa kwa mafanikio yetu.

Kwa muda ambao nimekuwa nawakochi watu kupiga hatua kwenye maisha yako, kila mara watu huwa wanakuja na vitu wanavyoamini ni vikwazo vya nje ambavyo vinawazuia kupiga hatua, lakini katika maongezi huwa naishia kugundua kwamba kikwazo kikubwa kwa mtu hakianzii nje, bali kinaanzia ndani yake mwenyewe.

Yaani hata kama nje ni pagumu kiasi gani, hata kama kila mtu anapitia changamoto ambayo unapitia, lakini sehemu kubwa ya kilichokukwamisha kinaanzia ndani yako mwenyewe.

Kabla sijaendelea kukueleza hilo kwa undani na hatua unazoweza kuchukua ili usikwame tena, tupate mfano wa mwanamafanikio mwenzetu aliyeshiriki programu ya GAME CHANGERS msimu wa juni 2019.

Ushuhuda GAME CHANGERS - MWANDEMUKA.jpeg

Kwanza kabisa ni shukrani na kuhusu programu hii (GAME CHANGES) imenijengea na kujifunza mambo yafuatayo;

  1. Kupungua kwa majukumu yangu ya kila siku. Hii ni kutokana na kuanza kuwatumia wafanyakazi wangu kwa kiasi kikubwa kwa majukumu niliyokuwa na lazimika kuyafanya kwa kila siku.
  2. Kuweza kuthubutu kuwa face wateja hata ambao sikuwa nawafikiria kabisa.
  3. Kutambua nimejikwamisha sana kwenye biashara yangu kwa muda sasa kwa kutokuwa na mfumo bora wa uebdeshaji biashara.
  4. Wafanyakazi hufanya kwa mazoea kama pia wewe unaendesha kwa mazoea.
  5. Masoko yapo kibwa zaidi ni kutokukata tamaa kwa majibu au ahadi unazokutana nazo katika kutafuta masoko

Hatua nilizoweza piga.

  1. Kuepuka kazi au wateja wenye usumbufu wa kulipa na hata kutofanya kazi  kabisa.
  2. Kupunguza matumizi ambayo sio ya lazima na kupanga budget ya mwezi na kuizingatia
  3. Kujifunza zaidi maarifa mbalimbali kwa kujisomea vitabu

Kuajiri watu wanaofaa katika biashara.

Asante.

Mwandemuka Kassim

Rafiki yetu Mwandemuka ameeleza kila kitu hapo kwenye ushuhuda wake kuhusu programu ya GAME CHANGERS.

Kwamba mara nyingi, mtu unakuwa umekwama kwa sababu ambazo zinakuwa zimeanzia ndani yako.

Wengi wamekuwa wanakimbilia kulaumu sababu za nje kama hali mbaya ya uchumi, ushindani kwenye biashara, wafanyakazi wasiojituma, kukosekana kwa wateja na kadhalika.

Lakini unapoingia ndani, unakuta ndiyo kuna vikwazo zaidi, mfano kukosekana kwa mfumo wa ufanyaji wa vitu, mtazamo hasi wa kwamba haiwezekani kupiga hatua, kufanya kwa mazoea, kuhofia kuwakabili watu ambao unapaswa kuwakabili na mengine mengi.

Rafiki, mpaka sasa unapaswa kuwa umeshapata jibu la kichwa cha makala hii, kilichokuvutia kuisoma, kwamba kuna mtu mmoja anayekuzuia wewe usifanikiwe zaidi, kama mpaka sasa hujamjua mtu huyo basi jibu ni wewe.

Wewe mwenyewe ndiye adui wa kwanza wa mafanikio yako. Mtazamo ulionao, fikra ulizonazo, tabia ulizonazo na jinsi unavyofanya mambo yako, kwa asilimia 80 kunachangia hapo ulipokwama sasa. Asilimia 20 pekee ndiyo inatoka nje yako.

Je unawezaje kutoka hapo ulipokwama sasa? Unawezaje kuacha kuwa adui wa mafanikio yako mwenyewe? Nimekuahidi jibu liko hapa.

Rafiki, inapofika wakati wa kujinasua kutoka pale ulipokwama, watu wengi hukimbilia kuanza na mambo ya nje, na haishangazi kwa nini hawafanikiwi kupiga hatua. Yaani wanaacha tatizo kubwa la ndani, na kuhangaika na tatizo dogo la nje.

Wewe unapaswa kuanzia ndani, na unapaswa kuanza na msingi mkuu kabisa ambao ni mabadiliko makubwa ya kimtazamo na kifikra, yaani kama ni simu au kompyuta basi unaiflash na kuweka upya programu kuu inayoiendesha.

Na njia pekee ya kufanya hivyo ni kuingia kwenye programu maalumu ya mafunzo na ukocha inayoitwa GAME CHANGERS. Hii ndiyo programu iliyomwezesha mwenzetu Mwandemuka kuweza kuvuka vikwazo vya ndani ambavyo vimekuwa vinaizuia biashara yake isikue zaidi. Na wewe itakusaidia kutoka hapo ulipokwama sasa.

Kuhusu programu hii ya GAME CHANGERS.

Rafiki, napenda kuchukua nafasi hii kukujulisha ya kwamba programu maalumu ya ukocha ya GAME CHANGERS itakuwa na msimu wake wa mwisho mwezi septemba mwaka huu 2019. Ni programu yenye nguvu kubwa ya kukusukuma na kukuwajibisha kuchukua hatua na hivyo kutokubaki hapo ulipo sasa.

Kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, unapata manufaa mawili kwa wakati mmoja, ambayo yana nguvu ya kukuwezesha kubadilika kabisa. Nguvu ya kwanza ni kuwa na kocha ambaye anakuongoza kwa karibu. Na nguvu ya pili ni kuwa pamoja na watu ambao nao wanabadilika. Katika kufanikiwa, vitu hivi viwili vimedhibitishwa kuleta matokeo bora sana, kuwa na kocha na kuzungukwa na watu ambao nao wanataka kufanikiwa.

Kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, nitafanya kazi kwa karibu na WATU WATANO tu kwa kipindi cha siku 30. Na ndani ya siku hizo 30 kutakuwa na mabadiliko makubwa sana, kila mtu atapata MPENYO wake wa ukuaji na baada ya siku hizo 30 mtu atatoka akiwa wa tofauti kabisa na ambaye ataweza kukua zaidi bila ya kujizuia yeye mwenyewe.

Kama kuna eneo lolote la maisha yako unaona umekwama, ambapo unajaribu kuweka juhudi sana lakini huoni matokeo ya tofauti, basi jua programu hii imekuja kwa ajili yako.

Kama ni kipato kimegoma kuongezeka kwa muda sasa, jua tatizo siyo kipato, bali tatizo ni wewe. Kama ni mahusiano yanakusumbua kwa muda sasa, jua tatizo linaanza na wewe. Na hata kama ni afya inakupa changamoto kwa muda, jua kuna namna ambayo fikra na tabia zako zinachangia hilo.

Karibu sana kwenye GAME CHANGERS ambayo utakwenda kutengeneza upya mfumo wa maisha yako, kuanzia fikra mpaka matendo, kitu ambacho kitakufungua sana. Kwenye programu hii utakwenda kuondoa kabisa breki ambazo unajiwekea wewe mwenyewe kwenye kupiga hatua zaidi.

UTARATIBU WA GAME CHANGERS.

Kwa kuingia kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, utapata nafasi ya kufanya kazi moja kwa moja na Kocha Dr Makirita pamoja na watu wengine wanne katika kutoka pale ulipokwama.

Utapata nafasi ya kujadili ulipokwama kwa kina na Kocha, na kisha kwa pamoja mtaweka mkakati utakaofanyia kazi kwa siku 30.

Utawekwa kwenye kundi maalumu la wasap la programu hii ambapo huko utakuwa pamoja na wengine wanaofanyia kazi mabadiliko kwenye maisha yao. Kundi hili litaendelea hata baada ya programu kumalizika.

Kila siku ya jumamosi, kuanzia saa 12 jioni kutakuwa na simu ya pamoja ya watu wote watano waliopo kwenye programu hii pamoja na kocha kwa ajili ya kupitia hatua ambazo kila mtu amepiga kwa juma zima. Katika simu hii ya pamoja, kila mtu anapata nafasi ya kumshauri mwenzake katika hatua anazochukua na changamoto anazokutana nazo.

Kila siku kwa siku 30 utapata somo moja la misingi ya GAME CHANGERS ambalo litakupa maarifa ya kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako. Kwenye kila somo na kila msingi, kutakuwa na mafunzo au kitabu cha rejea ambapo utaweza kujifunza kwa kina zaidi.

Kwa siku zote 30 za programu hii, una uhuru wa kuwasiliana na kocha katika muda wowote, kuuliza chochote na kupatiwa majibu au ushauri wa kitu sahihi kufanya kwa pale ulipokwama.

Unaweza kushiriki programu hii ukiwa sehemu yoyote nchini Tanzania, na ambapo una mtandao wa simu na mtandao wa intaneti.

ADA YA GAME CHANGERS NA TAREHE YA KUANZA.

Ada ya kushiriki kwenye msimu huu wa GAME CHANGERS SEPTEMBA 2019 ni tsh laki tatu (300,000/=) kwa mwezi mzima, ambayo ni sawa na uwekezaji wa tsh elfu 10 kwa siku.

Kwa uwekezaji huu ambao unaonekana ni mkubwa, utaweza kupata thamani ambayo ni mara kumi ya ulichowekeza. Ninakuhakikishia kwamba kama utajitoa kweli kwenye programu hii, basi utaweza kupata thamani mara 10 ya uwekezaji huo. Yaani kwa kiwango cha chini sana, matokeo utakayopata thamani yake itakuwa shilingi milioni 3.

Programu hii ya GAME CHANGERS itaanza rasmi tarehe 01/09/2019.

Ili kupata nafasi ya kushiriki programu hii unapaswa kulipa ada ya ushiriki, tsh 300,000/=.

Nafasi za kushiriki programu hii ni 5 pekee. Na nafasi zinatolewa kwa wale wanaowahi. Yaani nafasi zikishajaa hakuna tena nyingine itakayopatikana.

Hivyo nikushauri sana uchukue hatua mara moja unapopata ujumbe huu ili usikose nafasi hii. Kwa sababu programu hii inakuja mara chache sana na huu ni msimu wa mwisho wa programu hii kwa mwaka huu 2019.

Mwisho wa kutuma ada ili kupata nafasi ya kushiriki programu hii ni tarehe 29/08/2019. Na kwa wale watakaokuwa wamepata nafasi, siku ya tarehe 30/08/2019 nitakuwa na maongezi ya simu na kila mmoja ili kujadili kwa kina alipokwama na kuweka mipango ya kufanyia kazi.

Tarehe 31/08/2019 tutaanza rasmi programu yetu na siku hiyo jioni saa 11 tutakuwa na maongezi ya simu ya kwanza kwa ajili ya kutambuana na kupeana mikakati ya kila mmoja wetu.

Karibu sana kwenye GAME CHANGERS, programu pekee inayoweza kukutoa hapo ulipokwama sasa.

Kama una nia ya kushiriki kwenye programu hii, tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno GAME CHANGERS ili kujiwekea nafasi.

Naamini hutaiacha nafasi hii adimu sana kwako kuondoka kwenye mkwamo ikupite. Chukua hatua sasa ili uweze kufanikiwa zaidi na kuondoka hapo ulipokwama sasa.

Tuma ujumbe sasa kwenye wasap namba 0717396253 kujiwekea nafasi ya SIKU 30 ZA KUONDOKA KWENYE MKWAMO NA KUKUA ZAIDI.

MUHIMU; Rafiki, nafasi za kushiriki programu hii ni 5 pekee, ni nafasi chache mno na hazitaongezwa, na hii ni nafasi ya mwisho unayoweza kupata ya kushiriki programu hii kwa mwaka huu 2019. Hivyo usikilize moyo wako, kama unakuambia hiki ni kitu unachohitaji basi unakihitaji kweli, usiendelee kujichelewesha kukua zaidi. Tuma ujumbe sasa kwa wasap namba 0717396253 kujiwekea nafasi ya kuwa kwenye programu hii ya GAME CHANGERS kwa msimu hii.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha

PS; AHADI YANGU kwako wewe rafiki yangu ni hii, kwa kiwango cha chini kabisa, unakwenda kupata thamani ambayo ni mara kumi ya ada utakayolipa. Na kama hilo halitatokea basi utaniambia na nitakurejeshea ada uliyolipa. Kusudi langu la kwanza ni kukuona wewe unapiga hatua kabla mimi sijanufaika, hivyo kama hutanufaika, nikuhakikishie kwamba hutapoteza fedha yako. Tuma ujumbe sasa kwenye wasap namba 0717396253 ujiwekee nafasi yako ya kushiriki programu hii.