“It’s ruinous for the soul to be anxious about the future and miserable in advance of misery, engulfed by anxiety that the things it desires might remain its own until the very end. For such a soul will never be at rest—by longing for things to come it will lose the ability to enjoy present things.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 98.5b–6a

Ni siku mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi hii bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USISUMBUKE KWA MAMBO YAJAYO…
Tumekuwa tunapoteza muda wetu na nguvu zetu kwa kusumbuka na mambo ambayo bado hata hayajatokea.
Labda ni habari ambazo zimetabiri mambo yatakuwa magumu zaidi siku zinazokuja.
Na sisi tunapatwa na hofu kuhusu siku hizo, kitu ambacho kinatufanya tusahau kabisa kuishi leo.

Kama una hofu kuhusu kesho, kama muda wote unafikiria kesho itakuwaje na utaweza kuivukaje, hutapata muda wa kuishi leo.
Na kama hutaishi vizuri leo, basi hutakuwa na maandalizi bora ya kuikabili kesho kwa namna itakavyokuja.

Kama wastoa hatupaswi kuruhusu muda mzuri tulionao leo upotee kwa sababu tuna wasiwasi na kesho yetu.
Badala yake tunapaswa kukazana kuishi vizuri kwenye siku hii ya leo, maana ndiyo muda pekee tunaoweza kuuathiri.
Na kwa kuchagua kuishi leo, tunapata matokeo ya tofauti kabisa, na hata kama kesho itakuja vibaya kama inavyotabiriwa, basi tunakuwa na maandalizi mazuri.
Lakini pia tunajua tabiri nyingi, hasa za mambo kuwa mabaya huwa haziwi kweli, hivyo kuna nafasi nzuri ya mambo kwenda vizuri sana kesho, na hapo kuwa na wasiwasi leo hakuna msaada kabisa.

Lakini pia kama wastoa tunajua kwamba leo inaweza kuwa ndiyo siku yetu ya mwisho hapa duniani au kwenye kile tunachofanya au kwa wale tunaokutana nao.
Je ina maana gani kushindwa kutumia nafasi hii ya leo vizuri, kwa kuhangaika na kesho ambayo inaweza isiwepo kabisa?
Ishi siku yako kwa ubora leo, halafu rudia tena hivyo kesho na mara zote maisha yako yatakuwa tulivu na bora sana.

MUHIMU; Tupo kwenye juma la vipaumbele, kwa kutumia vizuri muda wetu kwa yale ambayo yanaingia kwenye mwongozo wetu wa #AfyaUtajiriHekima, karibu upate zawadi ya vitabu vya muda, kwa kulipa tsh elfu 5 unapata kitabu cha PATA MASAA MAWILI, ON THE SHORTNESS OF LIFE na uchambuzi wa kitabu hicho. Tuma fedha kwa namba 0717396253/0755953887 kisha tuma ujumbe wenye barua pepe yako na maneno ZAWADI YA MUDA, na utatumiwa.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchagua kuishi leo na kuachana na hofu za siku zinazokuja.
#IshiLeo #UsisumbukeNaYajayo #HofuHaijengi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1