“I was shipwrecked before I even boarded . . . the journey showed me this—how much of what we have is unnecessary, and how easily we can decide to rid ourselves of these things whenever it’s necessary, never suffering the loss.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 87.1
Tumeiona siku hii ya leo kama bahati kwetu,
Siyo kwa sababu tuna akili wana, au kwa sababu tunastahili sana,
Ila ni kwa sababu kazi yetu hapa duniani bado haijakamilika.
Hivyo leo tuna jukuku kubwa la kwenda kutekeleza majukumu yetu, kufanya yale ambayo ni muhimu kwetu. Tusipoteze hata dakika moja leo kwa yale yasiyo kuhimu.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Tusimamie hayo matatu na siku yetu itakuwa bora sana.
Asubuhi ya leo tutafakari MAJANGA YANACHOKUFUNDISHA…
Huwa hatupendi majanga, lakini kila janga huwa linakuja na somo kubwa sana kwetu, ambalo tusingelijua kama tusingekutana na janga hilo.
Fikiria upo kwenye usafiri wa meli, halafu unapewa taarifa kwamba meli hiyo imeanza kuzama, je utachukua hatua gani? Utaanza kuchukua mizigo yako na kuondoka nayo au kujiokoa wewe mwenyewe?
Au fikiria upo ndani ya nyumba umelala, ghafla unastuka nyumba inaungua moto, je utafanya nini? Utaanza kutoa kitanda chako nje ili kisiungue au utakimbia wewe mwenyewe kwanza?
Rafiki, kwa mifano hiyo miwili, unajionea wazi kwamba inapokuja kwenye swala la maisha na kifo, kitu pekee chenye umuhimu kwetu ni uhai wetu. Vingine vyote havina umuhimu mkubwa, ni vitu vya nyongeza tu, ambavyo tunaweza kuvipoteza na hata kuvipata tena.
Somo hapa ni hili, majanga yanatufundisha ni kitu gani muhimu zaidi kwetu. Kwa sababu kuna wakati tunajisahau, tunajikuta tunasumbuliwa sana na vitu ambavyo havina hata uzito, vitu ambavyo tupo tayari kuviacha pale uhai wetu unapokuwa hatarini.
Sasa ya nini turuhusu vitu hivi viharibu maisha yetu, vitutoe roho?
Kwa upande mwingine majanga yanatufunulia uwezo wetu. Huenda umekwama kwa sababu ya kitu ambacho umeshakizoea, kikiondoka ndiyo unaona mwanga wa nini unaweza kufanya.
Mfano watu wengi huwa wamezoea ajira na wanaona hawawezi kuziacha, lakini ikitokea wamefukuzwa kazi, ndiyo wanagundua kumbe wanaweza kuyaendesha maisha yao bila ya kazi hizo.
Rafiki, kila janga, ugumu au changamoto unayokutana nayo, jiulize inakufundisha nini na inakuonesha ubora upi uliopo ndani yako. Na kwa hakika utakuwa bora sana.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutumia kila janga unalokutana nalo kiyatafakari maisha yako na kuwa bora zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1