“Heraclitus would shed tears whenever he went out in public—Democritus laughed. One saw the whole as a parade of miseries, the other of follies. And so, we should take a lighter view of things and bear them with an easy spirit, for it is more human to laugh at life than to lament it.”
—SENECA, ON TRANQUILITY OF MIND, 15.2
Tushukuru kwa siku hii nyingine nzuri tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Aaubuhi ya leo tutafakari KUCHEKA AU KULIA?
Mambo tunayokutana nayo kwenye maisha huwa yanaibua hisia tofauti ndani yetu.
Kuna mambo yanayotufurahisha na hivyo tunaishia kucheka,
Lakini pia kuna mambo yanayotukasirisha na kutuhuzunisha na hivyo tunaishia kulia.
Hisia zote hizi huwa zinakuja moja kwa moja, kwa sababu ni tabia ambazo tumeshajijengea.
Lakini sisi kama wastoa, tunapaswa kuzuia hili la hisia kuja moja kwa moja, kwa kuchagua hisia ipi tutumie kwa wakati tunaotaka sisi.
Kwa sababu kucheka ni bora kuliko kulia, basi ni vyema tukajipa sababu ya kucheka kwa kila jambo.
Hata kama jambo lililotokea ni baya na linaloumiza, wewe angalia ndani yake na utaona kuna kitu cha kukuchekesha.
Na kwa hakika, ndani ya kila kitu au kila jambo, kuna kitu cha kuchekesha, ambacho unaweza kukitumia na kuepuka kulia.
Kulia ni hisia kali na zinazokuacha kwenye hali mbaya kuliko kucheka.
Epuka sana kuruhusu hisia zako zitokee zenyewe na kukupeleka kwenye hali kama hizo.
Badala yake dhibiti hisia zako kwa kuchagua mwenyewe utajibuje kihisia kwa yale yanayotokea.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchagua kucheka kwa kila jambi unalopitia au kukutana nalo kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1