Rafiki yangu mpendwa,

Mwaka wetu wa mafanikio kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni tofauti kabisa na miaka ya watu wengine. Sisi mwaka wetu huwa unaanza Novemba na kumalizika Oktoba ya mwaka unaofuata.

Tunaanza mwaka wetu wa mafanikio mapema ili kupata nafasi nzuri ya kuweka mikakati na kuanza kuifanyia kazi kwa hamasa kubwa wakati watu wengine wanakuwa wameshachoka na wanasubiria mwaka uanze ndiyo waanze na hamasa mpya.

Mwisho wa mwaka watu wengi wanakuwa wameshakata tamaa kwa malengo wanayokuwa wamejiwekea kwenye mwaka huo, lakini sisi kwenye KISIMA CHA MAARIFA tunakuwa ndiyo kwanza tunauanza mwaka mpya wa mafanikio.

DSC_0097
WANACHAMA WA KISIMA CHA MAARIFA KWENYE SEMINA YA MWAKA 2018
DSC_0101
WANACHAMA WA KISIMA CHA MAARIFA KWENYE SEMINA YA MWAKA 2018
DSC_0096
WANACHAMA WA KISIMA CHA MAARIFA KWENYE SEMINA YA MWAKA 2018

Mwaka huu wa mafanikio huwa tunauanza pamoja kwa semina kubwa ya mafanikio. Hii ni semina ambayo wanamafanikio wote kutoka pande zote za Tanzania wanakutana pamoja, kwa tukio la siku nzima, wakijifunza, kushirikiana na kuhamasishana ili kuondoka na hamasa ya kwenda kuchukua hatua zaidi.

Kukaa mwenyewe na kusoma ni hatua moja, kukutana na wengine ambao wanapambana ili kufanikiwa zaidi ni hatua nyingine yenye nguvu sana.

Nichukue nafasi hii kukukaribisha sana wewe rafiki yangu kwenye semina yetu kubwa ya kuumaliza mwaka wa mafanikio 2018/2019 na kwenda kuuanza mwaka wa mafanikio 2019/2020.

Semina hii itafanyika Jumapili ya tarehe 03/11/2019 jijini Dar Es Salaam. Unazipata taarifa hizi mapema kabisa ili uweze kufanya maandalizi mazuri, hasa kwa wale wanaosafiri. Muhimu ni kuhakikisha kwa namna yoyote ile, hukosi semina hii muhimu sana kwa mafanikio yako.

Napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja, tukijifunza na kuchukua hatua ili kuyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi.

Kwenye semina hii tutapata mafunzo ya kina kutoka kwa kocha Dr Makirita Amani, pia tutapata kujifunza kutoka kwa walimu wengine. Na sehemu muhimu zaidi ya semina hii ni kwamba tutapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wanamafanikio wenzetu, kupata shuhuda halisi za jinsi ambavyo wenzetu wanapiga hatua kwenye maisha yao.

Hii ni nafasi moja ya mwaka ambayo hupaswi kuikosa kwa namna yoyote ile, kwa sababu utajifunza na kuhamasika, kisha unaondoka na nguvu ya kwenda kuweka juhudi kwa mwaka mzima na kupiga hatua zaidi.

Semina hii inawakusanya wanamafanikio wote kutoka kila kona ya Tanzania na wengine kutoka nchi jirani, ambao wanakuja pamoja na kujifunza kwa kina kwa siku moja na kuondoka na nguvu na hamasa kubwa ya kuchukua hatua ili kufanikiwa zaidi.

Kwenye semina ya mwaka huu 2019 tutakwenda kupata shuhuda nyingi sana kutoka kwa wenzetu ambao wamepiga hatua mbalimbali, kuanzia walipotoka na jinsi ambavyo wameweza kupiga hatua kupitia maarifa wanayopata pamoja na huduma nyingine wanazopata kama huduma za ukocha.

Pia tutakwenda kujifunza kwa wale walishiriki huduma mbalimbali za ukocha na jinsi ambavyo wameweza kupiga hatua ambazo hawakudhani kama wangeweza kupiga.

Kwenye semina hii pia utapata nafasi ya kushirikisha ni hatua zipi umepiga kwa mwaka wa mafanikio 2018/2019 na kuahidi lengo moja kubwa unalokwenda kufanyia kazi mwaka wa mafanikio 2019/2020 mbele ya wanamafanikio wote.

Semina hii itakwenda kuwa nguvu kubwa sana kwako, itakwenda kuwa sababu ya wewe kujituma zaidi mwaka mzima, ili unaporudi tena kwenye semina ya kuuanza mwaka wa mafanikio 2020/2021 uwe na hadithi nzuri ya kuwashirikisha wengine kutokana na lengo kuu uliloahidi.

KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.

Ili kupata nafasi ya kushiriki semina ya kukutana ana kwa ana ya mwaka huu 2019, kwanza kabisa lazima uwe mwanachama hai wa KISIMA CHA MAARIFA, ambaye ada yake haijaisha.

Ukishakuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unapaswa kulipa ada ya ushiriki wa semina ambayo ni tsh 100,000/= (laki moja). Ada hii itajumuisha huduma zote utakazozipata kwa siku nzima ya semina, kuanzia kifungua kinywa, chakula cha mchana, vitafunwa vya jioni, vijitabu vya kuandika na kalamu.

Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, basi jiunge sasa ili uweze kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kujiunga utapata manufaa mengine mengi sana, ya kujifunza pamoja na kuwa kwenye klabu za mafanikio. Kujiunga, tuma ujumbe sasa kwa wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA na utatumiwa maelekezo ya kujiunga.

MWISHO WA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI.

Mwisho wa kupata nafasi ya kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 ni tarehe 31/10/2019, hivyo unapaswa kuwa umeshalipa ada yako ya kushiriki semina hii mpaka kufikia tarehe hiyo.

Ili kuhakikisha kila mtu anashiriki semina hii natoa nafasi ya kulipa ada kidogo kidogo ili mpaka kufikia tarehe 31/10/2019 uwe umeshakamilisha malipo yako.

Unaweza kuchagua kulipa yote tsh 100,000/= kwa mara moja mapema na hapo ukajiweka uhakika wa kushiriki semina.

Unaweza kuchagua kulipa kila mwisho wa mwezi tsh 35,000/= kuanzia mwisho wa mwezi wa nane, wa tisa na wa kumi na hapo utajihakikishia kushiriki.

Unaweza kuchagua kulipa kila mwisho wa wiki, na kila wiki ukalipa tsh 10,000/= na ukawa umemaliza malipo yako ndani ya muda huo.

Lakini pia unaweza kuchagua kulipa kila siku, kwa kulipa tsh 2,000/= na ukilipa kila siku ndani ya siku zilizobaki utajihakikishia kupata nafasi ya kushiriki semina yetu ya mwaka 2019.

HATUA ZA KUCHUKUA LEO ILI USIKOSE SEMINA HII.

Rafiki, ili kuhakikisha hukosi semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, basi chukua hatua hii sasa, andika ujumbe wa kawaida au wasap na tuma kwenye namba 0717396253, ujumbe uwe na majina yako kamili, namba yako ya simu, barua pepe yako na maelezo kwamba utashiriki semina. Pia kwenye ujumbe huo eleza kama utalipa ada kwa siku, wiki, mwezi au mara moja, na tarehe utakayofanya hivyo.

Mfano wa ujumbe ni kama hivi; mimi Makirita Amani, simu; 0717396253, email; makirita@kisimachamaarifa.co.tz Nitashiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, ada nitalipa kila tarehe ya mwisho wa mwezi.

Chukua hatua hiyo sasa rafiki yangu ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA mwaka 2019, kitu ambacho kitakupa msukumo mkubwa wa kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Asante sana rafiki yangu na nina uhakika tarehe 03/11/2019 tutakuwa pamoja kwenye semina, tuma ujumbe wako sasa wa kuthibitisha kushiriki ili usikose nafasi.

MUHIMU; Ili usisumbuke, thibitisha ushiriki wako mapema kwa kutuma ujumbe wenye majina yako, mawasiliano na mpango wako wa malipo.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha