“No person has the power to have everything they want, but it is in their power not to want what they don’t have, and to cheerfully put to good use what they do have.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 123.3
Ni siku mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi hii nyingine bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari TUMIA VIZURI ULICHONACHO…
Hakuna mtu yeyote mwenye nguvu ya kupata kila anachotaka kwenye maisha yake,
Hata uwe na uwezo kiasi gani, kuna vitu ambavyo utashindwa au havitakwenda kama unavyotaka.
Lakini kila mtu ana uwezo wa kutokutaka kile ambacho hana. Hata kama huna uwezo, ipo ndani ya uwezo wako kutokutaka kila ambacho huna.
Na pia unayo nguvu na uwezo wa kutumia vizuri kile ambacho kipo ndani yako, na kupata matokeo mazuri.
Maisha ya wengi ni magumu kwa sababu wanataka wapate kila kitu wanachokitaka, wanaangalia sana ni nini walichokosa na kusahau kabisa kile ambacho tayari wanacho.
Kama tukibadili hili, tukajua hatuwezi kupata kila tunachotaka, na kuacha kusumbuka na tusichokuwa nacho na kutumia vizuri kile ambacho tayari tunacho, tutaweza kupiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako.
Hangaika na kile unachoweza kukiathiri, na hicho ni kile kilicho ndani yako, siyo ulichokosa au unachotaka, bali kile ambacho tayari unacho.
Ukipeleka nguvu zako zote kwenye kile ambacho tayari unacho, utaweza kupiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutumia kile ambacho tayari unacho na kuacha kusumbuka na usichokuwa nacho.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1