“Anything that must yet be done, virtue can do with courage and promptness. For anyone would call it a sign of foolishness for one to undertake a task with a lazy and begrudging spirit, or to push the body in one direction and the mind in another, to be torn apart by wildly divergent impulses.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 31.b–32

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nzuri sana ambayo tumeiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UNAPOJISIKIA UVIVU KUFANYA KITU…
Huwa tunajiwekea malengo na mipango mbalimbali kwenye maisha yetu.
Lakini inapofika wakati wa utekelezaji ww mipango hiyo, tunakutana na upinzani fulani ndani yetu, ambao unatuzuia kufanya.
Tunapatwa na uvivu wa kufanya tulichopanga na kuishia kuahirisha kwa kujiambia tutafanya baadaye au bado hatujawa tayari.

Iweje wewe mwenyewe ukae chini na kupanga nini utafanya, na kwa wakati gani, halafu wakati wa kufanya unapofika uanze tena kujipa sababu badala ya kufanya?
Ni muhimu ukae chini na kujiuliza hilo.
Weka pembeni zile sababu ambazo umekuwa unajipa, kwamba huna muda, au hujawa tayari au utafanya baadaye.

Ukiweka pembeni sababu hizo na kuchimba ndani ili kupata sababu ya kweli, utagundua ukweli halisi.
Utagundua kinachokukwamisha ni hofu ulizonazo,
Labda una hofu ya kushindwa, hofu ya kukataliwa, hofu ya kudhalilika na nyinginezo.

Hii ina maana kama unataka kuondokana na uvivu au hali ya kuahirisha mambo, jua kabisa hofu ulizonazo, kisha jitoe kufanya licha ya kuwa na hofu hizo.
Usikubali kuacha au kuahirisha ulichipanga kufanya, wakati unapanga ulikuwa na akili timamu kabisa, usiruhusu hofu zikusukume kufanya maamuzi yasiyo sahihi kwako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutokuruhusu hofu iwe sababu ya wewe kutokutekeleza yale uliyopanga, ikabili hofu kwa kufanya kile unachohofia.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1