“Remember, then, if you deem what is by nature slavish to be free, and what is not your own to be yours, you will be shackled and miserable, blaming both gods and other people. But if you deem as your own only what is yours, and what belongs to others as truly not yours, then no one will ever be able to coerce or to stop you, you will find no one to blame or accuse, you will do nothing against your will, you will have no enemy, no one will harm you, because no harm can affect you.”
—EPICTETUS, ENCHIRIDION, 1.3

Ni siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari HANGAIKA NA YANAYOKUHUSU TU…
Kama unataka uhuru kwenye maisha yako,
Kama unataka utulivu mkubwa,
Kama hutaki kukasirishwa, kuangushwa au kukatishwa tamaa,
Kama hutaki kutegemea huruma za wengine,
Basi hangaika na yanayokuhusu tu.
Taka kile ambacho tayari unacho,
Usitamani kile ambacho huna,
Hangaika na kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako,
Na achana na vilivyo nje ya uwezo wako.

Kwa kuyaendesha maisha yako kwa msingi huu, hakuna yeyote anayeweza kukusumbua, wala chochote kukutesa,
Kwa sababu hakuna chochote unachotegemea, ambacho kipo nje ya uwezo wako.
Mateso wanayopata wengi kwenye maisha ni kwa sababu wanaweka mategemeo yao kwa watu wengine, na watu hao wanapoamua kuwanyanyasa, basi wanaumia kweli.
Hakuna anayeweza kukunyanyasa kama hakuna unachotegemea kwake.

Ishi maisha ya uhuru kamili, jitegemee wewe mwenyewe na hangaika na yale yanayokuhusu tu, taka kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako na usijisumbue na kile ambacho huna.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuhangaika na yale yanayokuhusu tu na kuachana na yaliyo nje ya uwezo wako.
#SumbukaNaYanayokuhusu #UsiweMtumwaWaWengine #TamaaYakoNdiyoInakuponza

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1