Rafiki yangu mpendwa,
Mwaka 2016 nilitoa kitabu kinachoitwa BIASHARA NDANI YA AJIRA, kitabu ambacho kililenga kuwawezesha waajiriwa kuanzisha biashara za pembeni wakiwa wanaendelea na ajira zao.
Sababu kubwa ni kwamba kipato cha ajira pekee hakitoshelezi, hivyo ili kuwa na uhuru wa kifedha, kila mwajiriwa anapaswa kuwa na njia mbadala ya kujiingizia kipato na kuacha kutegemea mshahara pekee.
Kitabu kilikuwa na misingi yote muhimu ya kuanzisha na kukuza biashara ukiwa bado umeajiriwa. Pia kikitoa majibu ya changamoto za wengi kama muda, mtaji na hata uzoefu wa biashara, kwa kuwa wengi ajira zinawabana.

Nikushukuru sana wewe rafiki yangu kwa sababu kitabu kilipokelewa vizuri na nakala zote zilizochapishwa za kitabu ziliweza kuisha kabisa. Watu wengi wamesoma kitabu hiki na kimekuwa msaada mkubwa sana kwao kuanzisha biashara zao wakiwa kwenye ajira na hata kuondoka kwenye ajira.
Kitabu hicho pia kimekuwa msaada kwa wale ambao hawapo kwenye ajira ila wapo kwenye biashara. Misingi muhimu ya kibiashara iliyopo kwenye kitabu hiki inaiwezesha biashara yoyote ile kukua.
Leo nakuandikia nikiwa na zawadi nzuri sana kwako kuhusu kitabu hicho cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.
Lakini kabla sijakueleza zawadi hiyo, nikupe taarifa kwamba ninaandaa toleo la pili la kitabu hiki, ambapo litakuwa bora zaidi ya toleo la kwanza. Toleo hili litakuwa na mafunzo zaidi kuhusu bishara na kikubwa zaidi, litakuwa na shuhuda za wale walioweza kufanyia kazi mafunzo ya toleo la kwanza na kuanzisha biashara zao.
Rafiki, nina zawadi nzuri sana kwako kama ulisoma kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA na ukachukua hatua za kuanzisha biashara yako ukiwa bado umeajiriwa.
Ili kupata zawadi hii, ninaomba unishirikishe ushuhuda wako wa jinsi kitabu hicho kilivyokusaidia kuanzisha biashara yako ukiwa kwenye ajira na mafanikio uliyopata kupitia biashara hiyo ya pembeni.
Ushuhuda unaotuma uwe kwenye mtiririko huu;
- Utambulisho wako kwa ufupi, majina yako, ulipo na kazi unayofanya.
- Maisha yako yalivyokuwa kabla hujasoma kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.
- Yale uliyojifunza kwenye kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.
- Hatua ulizochukua na biashara uliyoianzisha baada ya kusoma kitabu hicho.
- Changamoto ulizokutana nazo baada ya kuanzisha biashara yako na jinsi ulivyokabiliana nazo.
- Mafanikio uliyoyapata kwa kuanzisha biashara ukiwa kwenye ajira, kwa upande wa kipato, uhuru na kama umeweza kuondoka kwenye ajira yako na kusimamia biashara yako kikamilifu.
- Ushauri wako kwa wale ambao wapo kwenye ajira lakini hawana njia nyingine ya kuingiza kipato.
Ukishaandaa ushuhuda huu tafadhali nitumie kwa njia ya ujumbe wa wasap namba 0717396253 au kwa barua pepe; amakirita@gmail.com au maarifa@kisimachamaaarifa.co.tz
Ushuhuda wako utashirikishwa kwenye toleo la pili la kitabu hicho cha BIASHARA NDANI YA AJIRA na hivyo utaweza kuwasaidia wengi ambao wamekwama kama ulivyokuwa umekwama wewe.
ZAWADI UTAKAYOPATA.
Kwa wale ambao watatuma ushuhuda wao na ukapata nafasi ya kujumuishwa kwenye kitabu, basi watapata nakala ya kitabu ambacho kimewekwa sahihi na mimi mwandishi wa kitabu. Nakala hiyo ya kitabu utaipata bure kabisa na utatumiwa popote ulipo Tanzania.
Lakini zawadi kubwa zaidi unayokwenda kuipata ni pale ambapo ushuhuda wako unakwenda kuwa na manufaa kwa watu wengine, kuwasaidia wale ambao wamekwama na kuwawezesha kuwa na maisha bora.
Nakuomba sana rafiki yangu, uchukue muda wako leo na kujibu maswali hayo ya ushuhuda na unitumie. Chukua hatua hiyo leo kwa sababu tayari maandalizi ya kitabu yanaendelea na kinapaswa kutoka mapema.
Nasubiri kusikia kutoka kwako rafiki yangu, ushuhuda wako hata kama ni mdogo kiasi gani, jua una msukumo chanya kwa wengine, hivyo tushirikishe, usione ni kitu kidogo, kila kitu kina ukubwa ndani yake.
Asante sana.
Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha