“Try praying differently, and see what happens: Instead of asking for ‘a way to sleep with her,’ try asking for ‘a way to stop desiring to sleep with her.’ Instead of ‘a way to get rid of him,’ try asking for ‘a way to not crave his demise.’ Instead of ‘a way to not lose my child,’ try asking for ‘a way to lose my fear of it.’”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 9.40.(6)
Ni siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NJIA TOFAUTI YA KUOMBA…
Tumezoea kuomba kile ambacho tunakitaka,
Lakini siyo mara zote tunakipata.
Ili kukabiliana na hilo la matokeo tusiyopenda kutokea,
Badala ya kuomba kupata kile tunachotaka, tunapaswa kuomba kupata uimara wa kukabiliana na chochote kitakachotokea.
Badala ya kuomba maisha yawe rahisi, omba uwe na uimara wa kukabiliana na maisha magumu.
Badala ya kuomba kila mtu akubaliane na wewe na yeyote asikupinge, omba kuwa imara kupokea mapingamizi ya wengine bila ya kutetereka.
Badala ya kuomba usipoteze ulichonacho, omba kuweza kuishinda hofu ya kupoteza na kuwa na utulivu hata pale ulichonacho kinapopotea.
Onapoomba kwa namna ya tofauti, kwa kuzingatia kile ambacho kipo ndani ya udhibiti wako, matokeo yoyote unayoyapata unaweza kukabiliana nayo.
Lakini unapoomba kile tu unachotaka, unapokikosa unajiona kama usiye na bahati.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuomba kwa tofauti, kuomba nguvu za kukabiliana na matokeo yoyote yatakayotokea badala ya kuomba matokeo fulani.
#UsitakeKilaKituKiweUtakavyo #OmbaUimaraNaSiyoVitu #HangaikaNaUnayowezaKudhibiti
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1