“Remember that your ruling reason becomes unconquerable when it rallies and relies on itself, so that it won’t do anything contrary to its own will, even if its position is irrational. How much more unconquerable if its judgments are careful and made rationally? Therefore, the mind freed from passions is an impenetrable fortress—a person has no more secure place of refuge for all time.
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.48

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NGOME ILIYO SALAMA.
Ngome pekee iliyo salama kwako na inayoweza kukukinga na changamoto mbalimbali unazokutana nazo kwenye maisha ni akili isiyosumbuliwa na hisia.
Pale ambapo unaweza kudhibiti fikra zako na kutokuruhusu hisia zikuvuruge unakuwa kwenye ngome ambayo ni salama kabisa kwa maisha yako.

Kwa sababu ukiangalia, matatizo mengi ambayo watu wanapitia kwenye maisha yao, huwa yanaanzia kwenye hisia.
Labda mtu ana hisia za hasira na kuchukua hatua ambazo zinamgharimu baadaye.
Au mtu ana hisia za tamaa na kuchukua kitu ambacho siyo chake,
Au mtu ana hisia za chuki na hivyo kubeba vinyongo ambavyo vinamuumiza.

Changamoto kubwa kwenye hisia ni kwamba huwa zinaibuka zenyewe, hivyo kama hatutajifunza njia bora ya kuzidhibiti, kila wakati tutajikuta kwenye matatizo mbalimbali.
Kazana kudhibiti fikra zako na kutokuruhusu hisia zikutawale katika kufanya maamuzi, na hapo utapunguza changamoto nyingi unazopitia.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kudhibiti fikra zako na kutoruhusu hisia zikutawale katika kufanya maamuzi.
#NgomeSalamaNiAkili #DhibitiFikraZako #UsiendeshweNaHisia

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1