“Does the light of a lamp shine and keep its glow until its fuel is spent? Why shouldn’t your truth, justice, and self-control shine until you are extinguished?”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 12.15

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine mpya tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari ACHA WEMA WAKO UNG’AE…
Mshumaa unapowashwa kwenye chumba chenye giza, huwa unang’aa na kuangaza chumba kizima bila ya ubaguzi.
Huwa unatoa mwanga wake mpaka pale mshumaa huo unapoisha kabisa.
Hivi ndivyo unavyopaswa kuwa kwa dunia,
Wewe unapaswa kuwa mshumaa wa dunia kwenye wema,
Kwa kusimamia ukweli, haki, ujasiri na kujidhibiti mpaka siku ambayo utaondoka hapa duniani.
Ruhusu wema wako ung’ae na kuangaza maisha ya wengine.
Kwa wewe kuishi kwa misingi ya wema, siyo tu utanufaika mwenyewe, bali utawanufaisha wengine na kuwa mfano mzuri kwao kuweza kuishi kwa wema pia.

Haijalishi eneo lina giza kiasi gani, mshumaa ukiwashwa unaangaza.
Na wewe pia, haijalishi upo kwenye mazingira magumu kiasi gani, kwa kuishi kwa misingi ya wema, utakuwa nuru kwa wengine pia.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuangaza dunia kwa kuishi kwa misingi ya wema ambayo ni HEKIMA, HAKI, UJASIRI na KUJIDHIBITI.
#WemaHauozi #UpendoWaMshumaa #IangazeDunia

MUHIMU; Tumeanzisha mtandao wa kutoa mafunzo ya falsafa ya ustoa, unaweza kuutembelea kwa anwani http://www.ustoa.or.tz
Karibu sana tujifunze kwa pamoja falsafa hii bora kwa maisha ya utulivu.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1