“The person who does wrong, does wrong to themselves. The unjust person is unjust to themselves—making themselves evil.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 9.4

Ni siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UNAJIUMIZA MWENYEWE…
Unapofanya jambo kwa ajili ya kumuumiza mwingine, jua ya kwamba unajiumiza mwenyewe kukiko yule unayemlenga.
Hii ni kwa sababu sisi binadamu ni viumbe pekee ambao tuna utashi, na tunapofanya makosa, tunajua kabisa kwamba tumefanya makosa, na hilo halituachi tukiwa tunajisikia vizuri.

Kila mmoja huwa anajisikia vibaya baada ya kufanya jambo ambalo siyo zuri kwa wengine.
Iwe umeiba, umetukana, umedanganya au kufanya kingine kama hivyo, utaumia zaidi wewe kuliko yule uliyemfanyia.
Utajisikia vibaya, utakuwa na majuto, utajidharau na unaweza hata kuumwa kabisa.
Yote hayo yanatokana na nafsi yako kukusuta kwa yale mabaya unayokuwa umeyafanya kwa wengine.

Wale wanaosema moto uko hapa hapa duniani ni kwa sababu hii,
Kwamba chochote kibaya unachowafanyia wengine, kitakuumiza zaidi wewe kuliko hao wengine.
Hivyo kama kuna sababu moja ya wewe kuwa mwema kila wakati, ni kujiepusha kujiumiza wewe mwenyewe.
Na hapo utaweza kuwa mwema kwako na kwa wengine pia, na kuwa na maisha tulivu yasiyo na majuto.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa mwema kwa wengine ili usijiumize wewe mwenyewe.
#KuwaMwemaKwaWengine #UbayaUtakuumizaZaidiWeweMwenyewe #MalipoNiHapaDuniani

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1