Ni kukazana kuwa bora zaidi leo kuliko ulivyokuwa jana.

Hii ndiyo kazi yako kuu, ambayo ukiipa kipaumbele sahihi utaweza kupiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako.

Na utaweza kuwa bora zaidi leo kuliko jana kama utaitumia siku ya leo kujifunza vitu vipya na kuchukua hatua mpya kwenye maisha yako. Kisha kulifanya hili kuwa zoezi lako la kila siku.

Sasa, unapofanya kujiendeleza binafsi kuwa kazi yako kuu, ina maana vitu vingine vyote ni vya ziada. Hivyo hupaswi kuahirisha jukumu hili kwa sababu ya majukumu mengine.

Kujiambia kwamba hujifunzi vitu vipya kwa sababu huna muda au umebanwa inakuwa ni kujidanganya na kujipoteza. Kwa sababu hiyo ndiyo kazi yako kuu, inayopaswa kupewa kipaumbele cha kwanza, sasa iweje kuwe na vitu vingine vinavyopata nafasi zaidi ya jukumu hili?

Tunajua kwamba uwekezaji unaolipa kuliko mwingine wowote ni uwekezaji binafsi, uwekezaji ndani yako wa kuhakikisha unakuwa bora zaidi kila siku, unajifunza vitu vipya na kuchukua hatua mpya.

Kila kitu kipewe uzito unaostahili kwenye maisha yako, na kujiendeleza binafsi kunapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kwako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha