“Such behavior! People don’t want to praise their contemporaries whose lives they actually share, but hold great expectations for the praise of future generations—people they haven’t met or ever will! This is akin to being upset that past generations didn’t praise you.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.18

Hongera mwanamafanikio kwa kupata nafasi hii nzuri ya kuiona siku hii mpya ya leo.
Hii ni nafasi nzuri na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KUWA SHUJAA SASA…
Ni tabia ya binadamu kutokumsifia mtu kwa kile ambacho anakifanya sasa.
Wengi husifia wale ambao wameshapita, wale ambao walifanya makubwa huko nyuma.
Hivyo kama unafanya makubwa leo hii, wale wanaokuzunguka hawana msukumo wa kukusifia.
Lakini ikitokea umefariki, sifa nyingi sana zitakuja kwako na kwa yale unayofanya.
Vizazi vijavyo vitapewa sifa zako na kuendelea kuzisambaza.

Kutokana na hili, imekuwa rahisi kwa wengi kutengeneza mazingira ya kusifiwa siku zijazo.
Kuangalia ni kitu gani wanaweza kufanya sasa na kikawapa sifa siku zijazo.
Lakini hili ni kupoteza muda.
Usipoteze muda wako kufikiria sifa za wengine, iwe ni sasa au baadaye.
Badala yake peleka nguvu zako zote kwenye kuwa mtu bora kabisa unayeweza kuwa kwa wakati huu.
Kuwa shujaa wako mwenyewe leo na sasa, na siyo kuangalia kesho.
Fanya kilicho sahihi sasa, na siyo kuangalia siku zijazo.
Siku zijazo huna nguvu nazo,
Lakini wakati ulionao sasa, una nguvu kubwa ya kuutumia vizuri, nenda kaanze kuutumia sasa.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuchagua kuwa shujaa wako mwenyewe leo na siyo kusubiri mpaka siku zijazo.
#WeweNiShujaa #IshiKishujaaLeo #UsisubiriKisifiwaNaWengine

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1