“The best and the greatest number of authors have asserted that philosophy consists of three parts: the moral, the natural, and the rational. The first puts the soul in order. The second thoroughly examines the natural order of things. The third inquires into the proper meaning of words, and their arrangements and proofs which keep falsehoods from creeping in to displace truth.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 89.9

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ambayo tumeiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari VIPANDE VITATU VYA FALSAFA..
Falsafa ina vipande vitatu,
Kipande cha kwanza ni maadili, haya yanatusaidia kuishi kwa msingi sahihi.
Kipande cha pili ni asili, hii inatusaidia kujua jinsi ambavyo vitu vipo na jinsi vinavyofanya kazi.
Kipande cha tatu ni fikra, hii inatusaidia kufikiri sahihi na kufanya maamuzi bora.
Vipande vyote hivi vitatu vya falsafa vina lengo kuu moja, kutuwezesha kuishi maisha bora.

Hivyo kila wakati angalia ni maadili gani unayoyaishi, asili inayokuzunguka na fikra zinazotawala akili yako, hivi ndivyo vinavyokutengeneza wewe.
Vikiwa bora na wewe utakuwa bora, vikiwa hovyo na wewe utakuwa hovyo.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujijengea maadili mazuri, kuijua asili inayokuzunguka na kuwa na fikra sahihi ili uweze kuwa mtu bora.
#KuwaNaMaadiliMazuri #IjueAsiliInayokuzunguka #FikiriKwaUsahihi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1