“But I haven’t at any time been hindered in my will, nor forced against it. And how is this possible? I have bound up my choice to act with the will of God. God wills that I be sick, such is my will. He wills that I should choose something, so do I. He wills that I reach for something, or something be given to me—I wish for the same. What God doesn’t will, I do not wish for.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 4.1.89
Kuiona siku hii nyingine mpya ya leo siyo kwa sababu ya akili au nguvu zetu, bali ni kwa bahati na rehema.
Tumeipata siku hii nyingine bure kabisa, wakati wapo ambao walikuwa tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha waione siku hii lakini haijawezekana.
Hivyo ni wajibu wetu kuitumia siku hii vizuri, kufanya kilicho sahihi na kuweka vizuri vipaumbele vyetu.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari SIYO KWA MATAKWA YAKO…
Mambo yanatokea siyo kwa matakwa yako, bali kwa matakwa ya asili, kama ambavyo Mungu ametaka na amepanga mwenyewe.
Hivyo unaweza kuweka juhudi kubwa na kufanya kila unachopaswa kufanya, lakini matokeo yakaja tofauti kabisa na ulivyotegemea.
Katika hali kama hiyo usijiumize kwa matokeo uliyopata, kama umefanya kila ulichopaswa kufanya basi jua matokeo yamekuja kama asili ilivyotaka na siyo kwa matakwa yako mwenyewe.
Ukiacha kuiendesha dubia kwa matakwa yako utakuwa na utulivu mkubwa sana ndani yako.
Ukiacha kutaka kila kitu kiende kama unavyotaka wewe, hakutakuwa na chochote kitakachokuvuruga.
Na ukiwa tayari kuweka juhudi sahihi, lakini ukaweza kupokea matokeo yoyote yatakayokuja, hakuna kinachoweza kukukatisha tamaa.
Hakuna yeyote awezaye kupata kila anachotaka, kwa wakati anaokitaka na kwa namna anavyokitaka, hayupo.
Hii ni kwa sababu matakwa yetu siyo matakwa ya asili.
asili inajiendesha yenyewe kwa misingi yake na siyo kuangalia sisi tunataka nini.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukubaliana na matakwa ya asili na siyo kulazimisha kila kitu kiende kama unavyotaka wewe.
#DuniaHaiendiKwaMatakwaYako #AsiliInajiendeshaKwaMisingiYake #KazanaNaHatuaUnazochukuaNaSiyoMatokeoUnayopata
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1