“This is the very thing which makes up the virtue of the happy person and a well-flowing life—when the affairs of life are in every way tuned to the harmony between the individual divine spirit and the will of the director of the universe.”
—CHRYSIPPUS, QUOTED IN DIOGENES LAERTIUS, LIVES OF THE EMINENT PHILOSOPHERS, 7.1.88

Umeipokeaje bahati hii nzuri ya leo rafiki?
Kuiona siku hii mpya ni bahati sana kwako kwa sababu siyo kila aliyepanga kuiona jana ameweza kuiona leo.
Na wewe hujaiona kwa akili zako au ujanja wako, bali ni kwa bahati tu.
Njia nzuri ya kuipokea na kuitumia bahati hii kuweka vizuri na kusikamia vipaumbeke vyetu, kutokuruhusu muda wetu upotee kwa yale yasiyo muhimu.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NGUVU KUBWA KULIKO WEWE…
Mambo mengi ambayo tunajisumbua nayo kwenye maisha yetu, ni mambo ambayo yapo juu sana ya uwezo wetu.
Lakini tunasumbuka nayo kama vile sisi ndiyo tunaiendesha hii dunia.
Tunapanga ratiba zetu vizuri na kisha linatokea jambo linalozuia ratiba hizo na sisi tunaumia kama vile kuna makosa tumefanya.
Labda ulipanga kufanya kazi fulani, lakini ghafla mvua kubwa inanyesha, na hiyo inakuzuia wewe kufanya ulichopanga.
Haijalishi utajilaumu na kujiumiza kwa kaisi gani, huna nguvu ya kupanga mvua inyeshe au isinyeshe. Mvua inanyesha au kutokunyesha kutokana na nguvu kubwa ambayo iko juu sana ya uwezo wako.

Tafakari hii inatusaidia sana kuachilia yale ambayo tumeyashikilia na yanatutesa.
Inatuondoa kwenye yale ambayo yapo nje kabisa ya uwezo wetu lakini tunang’ang’ana nayo.
Kwa tafakari hii, tunasumbuka na yale tunayoweza kuyaathiri na kukubaliana na yale ambayo hatuwezi kuyaathiri.
Hivi ndivyo unavyoweza kuwa na maisha tulivu.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutambua kwamba wewe siye unayeiendesha hii dunia na hivyo kuacha kutaka kila kitu kiende kama ulivyopanga wewe.
#KunaNguvuKubwaKulikoWewe #KazanaNaYaliyoNdaniYaUwezoWako #DuniaHaiendiKamaUnavyotakaWewe

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1