“Remember that you are an actor in a play, playing a character according to the will of the playwright—if a short play, then it’s short; if long, long. If he wishes you to play the beggar, play even that role well, just as you would if it were a cripple, a honcho, or an everyday person. For this is your duty, to perform well the character assigned you. That selection belongs to another.”
—EPICTETUS, ENCHIRIDION, 17
Kuiona siku hii nyingine mpya na nzuri sana kwetu ni bahati,
Siyo kwa nguvu zetu wala akili zetu, bali ni kwa bahati tu.
Tunapaswa kuitumia siku hii vizuri, kwa kwenda kufanyia kazi vipaumbele vyetu na kuweks juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAISHA NI MAIGIZO…
Maisha ni kama sinema kubwa, na sisi binadamu ni waigizaji kwenye semina hii.
Kuna mwongozaji mkuu wa hii semina, ambaye anatupangia sisi ni nafasi zipi tuigize na kwa wakati gani.
Kuna wakati anatupangia kuigiza nafasi ya tajiri, wakati mwingine kuigiza nafasi ya masikini.
Kuna wakati anatupangia kuigiza nafasi ya ombaomba, wakati mwingine anatupangia nafasi ya uongozi.
Nafasi yoyote ambayo asili inakupa ucheze kwenye hili igizo la maisha, unapaswa kuipokea na kuicheza vizuri.
Kulalamika na kulaumu kwa hali fulani unazopitia hakuwezi kukusaidia kwa namna yoyote ile.
Unachopaswa kufanya ni kuigiza nafasi yako vizuri, kuitumia ile hali unayopitia vizuri na kuziona fursa nyingi zinazokuzunguka kwenye kila hali unayopitia.
Usitake maisha yaende kama unavyotaka wewe, wewe siyo mpangaji wa hili igizo.
Badala yake pokea kila nafasi unayopewa na itumie vizuri, huku ukiziona fursa zilizopo kwenye nafasi hiyo zinazoweza kukupeleka juu zaidi.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuigiza vizuri nafasi uliyopewa kwenye hili igizo la maisha na kuzitumia fursa zinazokuzunguka pale ulipo sasa.
#MaishaNiMaigizo #TumiaVizuriNafasiUliyonayoSasa #UsilalamikeWalaKulaumu
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1