“Meditate often on the swiftness with which all that exists and is coming into being is swept by us and carried away. For substance is like a river’s unending flow, its activities continually changing and causes infinitely shifting so that almost nothing at all stands still.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 5.23

Hongera mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KILA KITU KINABADILIKA…
Moja ya sababu zinazopelekea watu wengi kuwa na msongo na maisha ya kuvurugwa ni kutaka kila kitu kiendelee kuwa kama kilivyo sasa. Jambo ambalo haliwezekani kabisa, kwa sababu kila kitu kinabadilika.
Kama ambavyo maji yanatiririka kwenye mto, ndivyo maisha na kila kitu kinabadilika.
Wewe mwenyewe unabadilika kila siku,
Wanaokuzunguka wanabadilika,
Hali ya hewa inabadilika,
Mazingira nayo yanabadilika.

Kutaka kila kitu kiendelee kuwa kama kilivyo sasa kwa sababu tu umeshazoea hivyo ni kujiweka kwenye mazingira ya kuumia.
Kwa sababu haipo ndani ya uwezo wako kuzuia mabadiliko.
Badala yake, yapokee mabadiliko yoyote unayokutana nayo na kisha yatumie kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa.

Ukiweza kunadilika kabla ya mabadiliko itakuwa vyema kwako,
Kama itakubidi ubadilike kutokana na mabadiliko yanayoendelea siyo mbaya.
Lakini kama utaachwa nyuma na mabadiliko, utakuwa umejitengenezea njia ya wewe mwenyewe kushindwa.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuyapokea mabadiliko na kuyatumia kuwa bora zaidi.
#MabadilikoNiLazima #BadilikaKablaYaMabadiliko #UsipinganeNaMabadiliko

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1