Msaada ni moja ya njia ambazo tunaweza kuzitumia kuboresha mahusiano yetu na watu wengine.
Pale unapotoa msaada kwa wengine unaonesha kwamba unawajali, upo tayari kuwasaidia pale wanapokwama.
Pale unapoomba msaada kwa wengine unaonesha kwamba unawaamini, upo tayari kujiweka kwenye mikono yao pale unapokwama.
Ili mahusiano yawe bora, lazima yawe na pande zote za msaada, kuomba na kutoa.
Mahusiano ambayo upande mmoja unaomba msaada tu huwa yanakuwa magumu, kwa sababu upande unaoomba maada tu unajiona ni dhaifu na upande unaotoa maada tu unaona unatumika.
Kwenye maisha yako na kwenye yale mahusiano muhimu kwako, lazima ujue ni msaada gani unapata kutoka kwa wengine na wewe unaweza kuwasaidia nini.
Unapokataa kuomba maada au kutoa msaada, unajifungia kwenye uzio wako mwenyewe na unakosa fursa nzuri ya kuboresha mahusiano yako na wengine.
Msaada ni kiungo muhimu sana kwenye kuboresha kila aina ya mahusiano, kitumie vizuri kwa manufaa yako, kwa kuwa tayari kuomba na kutoa maada kwenye yale maeneo muhimu.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,