“For any challenge we should hold three thoughts at our command:
‘Lead on God and Destiny,
To that Goal fixed for me long ago.
I will follow and not stumble; even if my will
is weak I will soldier on.’”
—CLEANTHES
Tumepata bahati nyingine nzuri ya kuiona siku hii mpya ya leo.
Tunapaswa kuitumia bahati hii vyema, kwa kuweka vizuri vipaumbele vyetu na kutokupoteza muda kwa mambo yasiyo na maana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari FIKRA TATU ZA KUKABILIANA NA KILA CHANGAMOTO…
Changamoto hazitakoma kwenye maisha yetu, kila wakati na kila hatua tunayopiga tunakaribisha changamoto mpya.
Zipo fikra tatu zinazoweza kutusaidia kukabiliana na changamoto tunazokutana nazo.
1. Ni mpango wa Mungu na asili.
2. Ilipangwa kutokea hivyo tangu awali.
3. Nitapambana na kushinda, hata kama niko dhaifu, sitakubali kushindwa.
Unapoanza na fikra hizi, mtazamo wako unakuwa bora na unaweza kukabiliana na kila aina ya changamoto.
Kwanza hutafuti mtu yeyote wa kumlaumu au kulalamika,
Bali unapokea kila changamoto na moja kwa moja unakwenda kuitatua.
Na kwa kuwa changamoto hazitakoma, hii ni njia bora sana ya kukabiliana nazo.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuzipokea changamoto na kuwa tayari kuzifanyia kazi bila malalamiko wala lawama.
#ChangamotoHazinaUkomo #KulalamaHakutakusaidia #KubaliNaChukuaHatua
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1