Kama unajua kusoma lakini husomi vitabu huna tofauti na mtu asiyejua kusoma, hii ni kauli ambayo Mwandishi Mark Twain alinukuliwa kuitoa. Ni kauli ambayo imebeba ukweli ambao wengi huwa hawapendi kuuangalia na kuukabili.

Usomaji wa vitabu ndiyo njia rahisi, nafuu na ya uhakika ya kuwaibia wengine kile ambacho wanakijua. Ndiyo njia bora ambayo kila mtu anaweza kuitumia kujifunza chochote na akawa bora sana.

Lakini licha ya ubora na umuhimu huu wa kusoma vitabu, watu wengi wamekuwa siyo wasomaji wazuri wa vitabu. Na hili limekuwa chanzo cha wengi kukwama kwenye maisha, kwa sababu hawana maarifa mapya ya kuwawezesha kupiga hatua.

Watu wengi wamekuwa wanaendesha maisha yao kwa mazoea, wanafanya leo kile ambacho walifanya jana. Na hii ndiyo sababu biashara nyingi hazikui, watu wengi waliopo kwenye ajira kipato chao hakikui na hata changamoto za kimaisha haziishi.

Kabla hatujaendelea naomba ujiulize maswali haya matatu na ujipe majibu kwa uaminifu;

Moja; tangu umemaliza shule, umeshasoma vitabu vingapi?

Mbili; kwa mwaka mmoja uliopita umesoma vitabu vingapi?

Tatu; je kwenye kipato chako una bajeti ya kununua vitabu na maarifa zaidi?

Kama umejipa majibu ya maswali hayo kwa uaminifu, utakuwa umeona kwamba upo nyuma kwenye usomaji wa vitabu. Na hilo linachangia sana wewe kukwama hapo ulipo saa.

Njia pekee ya wewe kupiga hatua kwenye maisha ni kujifunza kupitia usomaji wa vitabu.

Lakini wengi wamekuwa wanashindwa kusoma vitabu kutokana na changamoto mbalimbali.

Leo nakwenda kukukaribisha kwenye programu bora ya usomaji wa vitabu ambayo inakwenda kujibu changamoto zote zinazokukwamisha kwenye usomaji wa vitabu.

CHANNEL YA SOMA VITABU TANZANIA.

SOMA VITABU TANZANIA ni channel iliyopo kwenye mtandao wa telegram. Channel hii inakupa vitabu vya kusoma pamoja na uchambuzi wa vitabu viwili kila wiki. Kwa kujiunga na channel hii, unapata uchambuzi wa vitabu wenye vitu vya kujifunza na hatua za kuchukua, lakini pia unapata vitabu vilivyochambuliwa, vyote kwa mfumo wa nakala tete (softcopy)

soma vitabu logo

Channel ya SOMA VITABU TANZANIA inaondoa changamoto hizi ulizonazo kwenye usomaji wa vitabu.

  1. Kukosa vitabu vya kusoma au kushindwa kuchagua vitabu vizuri kwako kusoma. Kupitia channel hii kila wiki utapata vitabu vizuri vinavyokuwezesha wewe kupiga hatua kwenye maisha yako.
  2. Kushindwa kusoma vitabu kwa lugha ya kiingereza. Kwenye channel hii utapata uchambuzi wa vitabu vizuri kwa lugha rahisi ya kiswahili ambayo unaweza kuielewa vizuri na kuchukua hatua.
  3. Kushindwa kupata vitabu kwa nakala ngumu (hardcopy) kutokana na kuwa mbali. Kwenye channel hii utapata vitabu kwa mfumo wa nakala tete (softcopy) ambapo unaweza kupakua na kusoma popote ulipo.
  4. Kushindwa kumudu gharama za kununua vitabu. Kwenye channel hii utapata vitabu na uchambuzi wake kwa kuanza bure, na baadaye kulipa ada ndogo sana ya tsh elfu moja, fedha ambayo umekuwa unatumia kununua vocha, lakini saa itakupa maarifa mengi ya kukuwezesha kupiga hatua.
  5. Kushindwa kuweka mtiririko wa vitabu ulivyosoma na kuwa na rejea ya haraka. Kupitia chambuzi za vitabu utakazozipata kwenye channel hii, utaweza kuwa na mtiririko mzuri wa vitabu ambavyo umevisoma na hata kuwa na rejea pale unapohitaji kufanya hivyo.

Rafiki, kwa hayo na mengine mengi utakayoyapata kwenye channel hii ya SOMA VITABU TANZANIA, utakuwa na uhakika wa kupata maarifa kila siku na kuweza kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.

JINSI YA KUJIUNGA NA CHANNEL YA SOMA VITABU TANZANIA.

Channel hii ipo kwenye mtandao wa telegram, hivyo kujiunga nenda kwenye telegram na tafuta SOMA VITABU TANZANIA au tumia kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania

Kama huna app ya Telegram kwenye simu au kompyuta yako, nenda kwenye playstore na tafuta TELEGRAM MESSENGER kisha ipakue na kuweka kwenye simu yako, andikisha namba yako ya simu kama unavyofanya kwa wasap na hapo utaingia na kuweza kuitafuta channel na kujiunga nayo.

Unapoingia kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa mara ya kwanza, bonyeza sehemu imeandikwa JOIN THIS CHANNEL na hapo utakuwa umejiunga.

ADA YA KUWA KWENYE CHANNEL HII.

Kujiunga na channel hii ni bure kwa wiki moja, baada ya hapo utapaswa kulipa ada ili uendelee kubaki kwenye channel na kunufaika na chambuzi za vitabu.

Ada inalipwa kwa mwezi au kwa mwaka.

Kiwango cha ada ni tsh elfu tano (5,000/=) kwa mwezi au tsh elfu hamsini (50,000/=) kwa mwaka.

Ada ya mwezi unalipa kila tarehe ya mwezi ambapo ada ya inamaliza muda wake. Ada ya mwaka unalipa baada ya ada ya awali kumaliza muda wake, yaani mwaka mzima.

Kwa kulipa ada ya mwaka unakuwa umeokoa ada ya miezi miwili.

Namba za kufanya malipo ya ada ya channel ya SOMA VITABU TANZANIA ni 0752 977 170 au 0678 977 007 majina ya namba zote mbili ni AMANI MAKIRITA. Ukishalipa ada unatuma ujumbe wenye majina yako kwa telegram kwenda namba 0678 977 007 ukiwa na maelezo kwamba umelipa ada ya SOMA VITABU TANZANIA.

Karibu sana kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA, tujifunze pamoja kupitia usomaji na uchambuzi wa vitabu. Fungua www.t.me/somavitabutanzania kujiunga na channel hii sasa.

www.t.me/somavitabutanzania