“A good isn’t increased by the addition of time, but if one is wise for even a moment, they will be no less happy than the person who exercises virtue for all time and happily passes their life in it.”
—CHRYSIPPUS

Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MARA MOJA INATOSHA…
Kinachopelekea watu kutengeneza uteja, ulevi na uraibu kwenye maisha yao, ni kwa sababu huwa hawaridhiki na kitu mara moja.
Huwa wanataka waendelee kupata raha ya kitu mielele, kitu ambacho hakiwezekani kwetu binadamu.

Kwa wenye busara, kupata kitu mara moja inatosha kabisa.
Kupata furaha kubwa mara moja, hata kama ni kwa muda mfupi hiyo inatosha kabisa.
Kwa sababu haina tofauti pale unapoipata furaha na kama utaendelea kuwa nayo.

Ni sawa na kushinda medani fulani, ile raha ya kushinda medani hiyo ni ya mara moja. Lakini medani utakaa nayo milele, hata kama raha ile hutakaa nayo kila siku
Hivyo ndivyo maisha yalivyo, hakuna kinachiweza kutupa raha ya kudumu wakati wote.
Hivyo lengo letu ni kuipokea furaha kwa wakati inapokuja na kuwa tayari pale inapoondoka. Tusitake kung’ang’ana ibaki, badala yake tuitumie wakati tunayo.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutumia nyakati za raha na furaha tunazopitia na kutokutaka zidumu milele.
#HakunaFurahaYaKudumu #PokeaKilaHaliKamaInavyokuja #MaraMojaInatosha

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1